Stori za Ghost: Jamaa ajisalimisha kwa polisi baada ya mahindi aliyokuwa ameiba kukwama kichwani

Jamaa huyo alipozidiwa na uzito wa gunia hilo aliamua kujialimisha kwa polisi ili kupata usaidizi.

Muhtasari

•Gunia hilo lilikwama kwenye shingo la jamaa huyo na kukatalia pale licha ya juhudi zake kujaribu kuiweka chini.

Ghost Mulee

Uchawi?

Katika kitengo cha story za Ghost alisimulia kisa cha jamaa mmoja aliyeshindwa kuweka chini gunia la mahindi alilokuwa ameiba;-

Soma simulizi:-

Jamaa mmoja maeneo ya Muranga anadaiwa kujisalimisha kwa polisi baada ya kushindwa kuweka chini gunia la mahindi ambalo alikuwa ameiba. 

Gunia hilo lilikwama kwenye shingo la jamaa huyo na kukatalia pale licha ya juhudi zake kujaribu kuiweka chini.

Jamaa huyo alipozidiwa na uzito wa gunia hilo aliamua kujialimisha kwa polisi ili kupata usaidizi.

Polisi walianza kumtafuta mwenye mahindi ili aweze kumtoa jamaa huyo mzigo ule.

Jamaa mwingine anadaiwa kuongeleshwa na gunia gunia la makaa alilokuwa ameiba kando ya barabara maeneo ya Voi.

Gunia hilo lilimwambia alirejeshe Voi alikoitoa.