Niliua chura wa nyanya yangu aliyekuwa anamtumia kuroga watu-Mwanamume atoboa siri

Muhtasari
  • Kuku wakiwa wwngi huwa wanamwaya mtama saa kumi ni moja na dkika hamsini kwenye kitengo cha toboa siri
  • Mwanamume mmoja alitoboa siri jinsi nyanya yake amekuwa akimtumia chura na nyoka ili kuwaangamiza watu
Lion,DJ Nyc na Mbusi
Image: Studio

Kuku wakiwa wwngi huwa wanamwaya mtama saa kumi ni moja na dkika hamsini kwenye kitengo cha toboa siri.

Mwanamume mmoja alitoboa siri jinsi nyanya yake amekuwa akimtumia chura na nyoka ili kuwaangamiza watu.

Licha ya hayo yote jamaa huyo alimtobolea nyanya yake siri na kumwambia kwamba chura ambaye amekuwa akimtafuta ni yeye alimuua.

Usimulizi

"Nyanya yangu amekuwa akimtumia chura na nyoka ili kuwaangamiza watu kwa muda mrefu sasa,amekuwa akiangamiza masomo ya watoto wa wenyewe na hata kazi baada ya kuchukua pesa zao

Chura amekuwa akiishi kwenye chumba chake cha kulala, na nyoka amekuwa akiishi msituni, kuna wakati nilipatana na chura huyo ambaye alikuwa anataoshana kama 'Ga boots' na nikamuua

Nyanya yangu amekuwa akimtafua lakini hajui kama nimemuua, nataka kumtobolea siri nimwambie kwamba ni mimi nilimuua

Pia nataka ushauri kwa wanajambo kama naweza muua nyoka ambaye amekuwa akiishi msituni,"