Tazama picha za mwanamke aliyepigwa risasi na mumewe Kiambu

Muhtasari
  • Tazama picha za mwanamke aliyepigwa risasi na mumewe Kiambu

Hali ya hofu ilitanda katika maeneo ya Kirigiti kaunti ya Kiambu baada ya wanandoa wawili kupatikana wameaga dunia nyumbani kwao Jumanne jioni.

Polisi walipata miili ya mwanabiashara Jonathan Mukundi Gachunga (42) na mkewe Philomena Njeri (30) ilipatikana ndani ya chumba chao cha kulala baada ya rafiki wao wa karibu kuwafahamisha kuwa Gachunga hakuwa anashika simu zake, jambo ambalo si la kawaida.

Kulingana na ripoti ya polisi, Mukundi ambaye ni mmiliki wa bunduki kihalali alimpiga mkewe risasi tatu kabla ya kujitoa uhai kwa kujipiga risasi kichwani.

Bastola ya mwanabiashara huyo ilipatikana katika eneo la tukio.

Hizi hapa baadhi ya picha za mwanamke

Philomena
Image: Hisani