"Hata nikifa, lazima nife nikiwa mwenye raha" Akothee asema huku akiendelea kupokea matibabu hospitalini

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto watano amelazwa katika wadi ya wagonjwa maarafu katika hospitali moja nchini.

•Mwanamuziki huyo ameendelea kupokea wageni mbalimbali pale hospitalini  haswa wa familia yake

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri nchini Esther Akoth almaarufu kama Akothee angali anaendelea kupokea matibabu hospitalini ambako alilazwa mwishoni mwa wiki iliyopita kufuatia maradhi yasiyotambulishwa.

Mama huyo wa watoto watano amelazwa katika wadi ya wagonjwa maarafu katika hospitali moja nchini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee ameonyesha hali ya kifahari ya chumba alicholazwa huku akionekana akihudumiwa na wauguzi maalum.

Kando na kitanda cha wagonjwa chumbani kile pia kina kabati kubwa, meza na viti vya wageni aina ya sofa na eneo la kupikia.

"Hata kama nitakufa, lazima nife nikiwa mtu mwenye raha" Akothee ameandika kuashiria kuwa anafurahia mandhari ya wadi aliyolazwa.

Mwanamuziki huyo ameendelea kupokea wageni mbalimbali pale hospitalini  haswa wa familia yake.

Mamia ya mashabiki wake wameendelea kumtumia jumbe za kumtakia afueni ya haraka.