"Nafaa kuwa hospitali!" Akothee afichua hajakuwa akihisi vizuri kwa muda

Muhtasari

•Msanii huyu mwenye umri wa miaka 41 amedai kwamba amekuwa akumia kwenye mkono wake wa kushoto.

•Amesema kuwa ingawa mkono wake umeishiwa na nguvu,  angali anaendelea na kazi zake kwa kuwa anajitegemea mwenyewe na lazima atimize malengo yake.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki na mfanyibiashara Esther Akoth almaarufu kama Akothee amefichua kuwa mgonjwa kwa muda sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyu mwenye umri wa miaka 41 amedai kwamba amekuwa akumia kwenye mkono wake wa kushoto.

Akothee amesema kuwa amekuwa akiumwa sana haswa masaa ya usiku anapoenda kulala

"Mkono wangu wa kushoto umepoteza nguvu. Nashuhudia uchungu mwingi  usiku... Usiku wangu umekuwa mrefu na vile vile mchana umekuwa mrefu" Alisema.

Mama huyo wa watoto watano amesema kuwa ingawa mkono wake umeishiwa na nguvu,  angali anaendelea na kazi zake kwa kuwa anajitegemea mwenyewe na lazima atimize malengo yake.

"Ukiniona nafanya kazi ni kwa sababu najitegemea mwenyewe na lazima  nitimize malengo yangu, nafaa kuwa hospitalini. Hata mimi napitia mambo fulani msinipe presha" Akothee alisema.

Aliambatanisha ujumbe wake na video iliyoonyesha akiwa anahudumiwa hospitalini huku akiwa amefungwa kwenye mkono wake wa kushoto.

Mashabiki wake wameendelea kumtumia jumbe za kumfariji huku wakimtakia kupona kwa haraka.