Mbona ulichumbiwa bila kuniambia?-Mike Sonko amuuliza Natasha huku akimpongeza

Muhtasari
  • Mike Sonko ampongeza Lucy Natasha baada ya kuvishwa pete ya uchumba
Image: FACEBOOK// MIKE SONKO

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko amempongeza Mchungaji Lucy Natasha baada ya kuchumbiwa na mpenzi wake, Prophet Stanley Carmel.

Mhubiri huyo wa Kenya alipata karamu ya aina yake ya uchumba katika hoteli ya Boma jijini Nairobi alipopata kumtambulisha mpenzi wake wa Kihindi kwa mara ya kwanza.

 Baada ya kujua kuhusu pendekezo hilo, Sonko alienda kwenye mtandao wa kijamii na ujumbe wa kuchekesha huku akiwapongeza wanandoa hao kwa kupata mapenzi.

Mwanasiasa huyo alimuuliza Natasha kwa nini hakumjulisha kuhusu mipango yake ya uchumba licha ya historia yao pamoja.

"Rev. Dr. Natasha why are you getting engaged without informing me naunajua vile tumetoka far ??????????Ama nisimamishe hiyo wedding ikifika. 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣Anyway congrats. Just kidding," Aliandika Sonko.