Willy Paul ananichukia kwa sababu niko mbele yake-Diana Marua adai

Muhtasari
  • Willy Paul Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, alimkejeli Diana huku akipigia debe albamu yake mpya
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Diana B amemjibu Willy Paul kwa kukosoa kuingia kwake katika ulimwengu na tasnia ya muziki.

Diana Marua maafufu Diana B kama anavyojiita anasema Pozze ana wivu tu kwani amefikisha watazamaji milioni moja ndani ya siku 3 tu, jambo ambalo anajaribu kufanya kwa sasa.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Jalang'o na Kamene Goro kwenye kipindi cha The Morning Kiss, Marua alisema;

"Nimetoa wimbo na tayari umetazamwa mara milioni 1 ndani ya siku 3 tu. Huyu jamaa amekuwa kwenye tasnia kwa muda mrefu. Bado nimejiunga na muziki kwa siku 3 tu. iliyopita. Nahisi anachukia kwa sababu niko mbele yake na amekuwa akifanya hivi kwa miaka mingi

KIba kingine kinatoka leo, Diana B yuko hapa kubaki. Na hii sasa ni mbayaa nangoja tu jeshi la Twitter sasa wakuje watupatie say.

Niliandika hatutaachana miezi miwili iliyopita na mwezi mmoja baadaye nilifanya hii ninayoitoa leo na inatoka moyoni mwangu na inazungumzia maisha yangu," Alisema Diana.

Willy Paul Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, alimkejeli Diana huku akipigia debe albamu yake mpya.

"Umechoka kusikiliza muziki mbaya kutoka kwa familia hiyo? Familia ya manduru na ma off-keys?? Najua wengi wenu bado mmepatwa na kiwewe coz of that ka tukio.

Usijali nimekufunika na tayari kukusaidia. Nenda kasikilize #theafricanexperiencealbum kwenye @boomplaymusicke sasa, nishukuru baadaye. Kwa mara nyingine tena samahani ulilazimika kupitia hayo yote, albamu yangu itakuponya."