Usinilazimishe nife kabla ya wakati wangu-Akothee kwa wanaosema ameaga dunia

Muhtasari
  • Usinilazimishe nife kabla ya wakati wangu, haya ni matamshi yake msanii maarufu Akothee, kwa watu wanaosema ameaga dunia.
Esther Akoth

Usinilazimishe nife kabla ya wakati wangu, haya ni matamshi yake msanii maarufu Akothee, kwa watu wanaosema ameaga dunia.

Esther Akothee almaarufu madam boss ni mwanamuziki na mjasirimali ambaye anafahamika sana nchini kutokana na bidii ya kazi yake.

Yeye pia ni mama wa watoto watano.

Katika muda wa mwezi mmoja uliopita Akothee amekuwa akilazwa hospitali huku akiruhusiwa kuenda nyumbani.

Yote yalianza pale alipolazwa kutokana na maambukizi ya mkono ambayo baadaye yalikua makubwa baada ya muda.

Baada ya dawa aliruhusiwa na baada ya wiki mbili alirudi tena hospitalini. Hata hivyo, hajafichua ugonjwa anaougua.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instaram msanii huyo ameonekana kugadhabishwa na watu ambao wanasema kwamba ameaga dunia.

Akothee amewaambia kwamba wakati wake haujafika, na wanapaswa kuacha hayo.

"R.I.P ? 🤔Usinilazimishe nife kabla ya wakati wangu. Sijachukua nafasi yako yoyote katika ulimwengu huu 🙏Acha kuandika R.I.P yangu mapema hivi .

Bado niko hai na Mungu anakusudi la mimi kuiona siku nyingine. Hata nikifa leo, Hakutakuwa na mbadala wa MALKIA MWENYE NGUVU MFALME AKOTHEE. LIVE MADAMBOSS 💪 Kifo hakiepukiki, sote tutakufa siku moja, tofauti pekee itakuwa 👉 asili ya kifo 👉Wakati 👉Sherehe ya mazishi 👉Ukubwa wa umbo na mtindo wa jeneza . Sasa kabla ya kunipeleka kwenye Kaburi la Mapema. Umewafanyia nini wanadamu ambacho umeacha kama urithi 🙏 ISHI KWA MUDA MREFU KWENU WOTE," Akothee alisema.