"Mimi ni bure kama mabaki!" Akothee ataja mambo ambayo ugonjwa anaougua umemzuia kufanya

Muhtasari

•Amesema katika kipindi hiki cha sikukuu hana uwezo wa kujiburudisha kwa njia mbalimbali ikiwemo kukata maji, kushiriki tendo la ndoa, kuenda kilabu pamoja na kupokea simu. 

•Amewapa kibali wanadada ambao wanammezea mate mpenziwe kutumia fursa hii kujipendekeza kwake akisema yeye hana uwezo mkubwa kwa sasa.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki na mfanyibiashara mashuhuri Esther Akoth almaarufu kama Esther Akoth ameweka wazi kwamba bado anaendelea kupata matibabu kufuatia ugonjwa ambao umemwathiri kwa kipindi kirefu sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanamuziki huyo amefichua kuugua kwake kumemzuia  kufanya mambo mbalimbali aliyokuwa anafanya hapo awali.

Mama huyo wa watoto watano amesema katika kipindi hiki cha sikukuu hana uwezo wa kujiburudisha kwa njia mbalimbali ikiwemo kukata maji, kushiriki tendo la ndoa, kuenda kilabu pamoja na kupokea simu. 

"Ukiwa unashangaa wapi pa kwenda na jinsi ya kusherehekea, kumbuka waziri wa burudani Madamboss SIBUOR MADHAKO leo anapanga madawa ya asubuhi, mchana na usiku wa manane.  Hii ni kiashiria wazi kuwa hakuna pombe, hakuna klabu, hakuna ngono, hakuna kupokea simu kutokana na mionzi" Akothee alisema.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 41 aliwaonya marafiki wake wanaume dhidi ya kumpigia simu na kumwita majina matamu katika kipindi hiki huku akieleza kuwa kwa sasa mpenzi wake Nelly Oaks ndiye anayepokea simu na SMS zote kwa niaba yake.

Isitoshe Akothee amewashauri wanadada ambao wanammezea mate mpenziwe kutumia fursa hii kujipendekeza kwake akisema yeye hana uwezo mkubwa kwa sasa.

"Kwa marafiki wangu wote wanaume, sina simu yangu. Nelly Oaks anapokea simu na sms zote, siko sawa kwa mazungumzo. Kutokana na maumivu ya kichwa ninayopata, huenda nisiwe na nafasi ya kumueleza kwa nini tunaitana hivyo! Huyu jamaa anaweza kunichukulia! Na sisi sote tunajua hamuwezi kuja kuwa nami hapa. Itabidi pia umjibu mke/mpenzi wako unaenda wapi. Ngoja nipone na nianze kukimbia, ili tuendelee kutoka tulipoachia.

 Usiudhike nisipopokea simu .Mionzi inanikera ,vibaya na kusababisha maumivu makali ya kichwa. Nelly atajibu simu zako zote. 

Kwa rafiki zangu wa kike wanaomtaka Nelly , huu ndio wakati, piga  hatua sasa kipenzi. Mpenzi ana vifaa vyangu vyote. Sina maana kama mabaki" Akothee aliandika.

Mwanamuziki huyo amekuwa akiugua kwa kipindi cha miezi kadhaa ambacho kimepita.

Hivi majuzi alitangaza kwamba amelazimika kulazwa hospitalini kwa mara ya tano kufuatia maumivu.