'Maisha yake yako hatarini anahitaji matibabu,'Eric Omondi azungumza baada ya polisi kuvamia afisi za Jimmy Wanjigi

Muhtasari
  • 'Eric Omondi azungumza baada ya polisi kuvamia afisi za Jimmy Wanjigi

Kinyang'anyiro cha kiti cha urais kinazidi kushika kasi huku Agosti ikija ikiita wanaotaka kufanya mikutano ya hapa na pale kama vile ya jana ya Eric Omondi na Jimmy Wanjigi hata hivyo hawakuchukua mkondo waliotarajia.

KUpitia kwenye mitandao ya kijamii ua  mchekeshaji mwenye utata ambaye anaongoza timu ya kampeni ya wanasiasa alifichua kuwa Kikosi cha polisi kilivamia kambi ya mkutano wao nje ya makao makuu ya Jimmy wakati mkutano ukiendelea.

Polisi waliwatawanya kundi la vijana waliokuwa wamesafirishwa hadi nje ya ofisi ya mfanyabiashara Jimi Wanjigi.

Wengine walikuwa wamefika ndani ya mabasi matatu na kabla ya wale waliokuwemo kushuka, gesi za kutoa machozi zilipigwa na kuwalazimisha madereva kuondoka kwa kasi.

Polisi walisema baadhi ya waliokuwa katika kundi hilo walikuwa wakiwaibia wananchi waliokuwa wakitembea kwa miguu na madereva wa magari.

Wanjigi alikuwa bado amejificha ndani ya ofisi yake kufikia saa nne unusu asubuhi.

Polisi kutoka DCI Kitengo cha Kupambana na Ugaidi wamekita kambi katika ofisi za Wamjigi tangu Jumatatu usiku.

Huku ERic akizungumzia kisa hicho alisema kwamba hawezi amini kwamba haya yanatendeka kenya.

Pia alifichua kwamba kuna mfanyikazi mwenzake ambaye anahitaji matibabu ya haraka, ilhali madaktari hawaruhusiwi kuingia ndani.

"Siwezi kuamini kuwa haya bado yanafanyika mwaka wa 2022. Hii ni Aibu kwa Kenya na Afrika kwa Ujumla. Watu katika Kiwanja hiki wamekabiliwa na Masharti ya Kinyama zaidi

Hawajala chochote kwa masaa 16. Kuna mwanadada mwenzetu maisha yake yako Hatarini kwa sababu anahitaji kutumia Dawa yake

Daktari yuko hapa nje na hangeruhusiwa kuingia. Tunawaomba atleast wamtoe ili apate UHAKIKI WA MATIBABU. Bosi wangu @jimi.wanjigi amekuwa akiomba aina yoyote ya Order au Warrant bila mafanikio," Aliandika Eric.