Kwa nini muoane? Wanamitandao watoa hisia tofauti kuhusu talaka kati ya Ali Kiba na mkewe

Muhtasari
  • Amina aliwasilisha kesi hiyo ya talaka katika mahakama ya Kadhi ya Mombasa mwezi jana baada ya miaka mitatu  kwenye ndoa
Ali Kiba na mkewe Amina
Ali Kiba na mkewe Amina
Image: hisani

Baada ya uvumi kuenea kuwa mkewe staa wa bongo Alikiba, Amina amewasilisha kesi mahakamani ya kutaka talaka kutoka kwa mumewe, wanamitandao walitoa hisia tofauti

Amina aliwasilisha kesi hiyo ya talaka katika mahakama ya Kadhi ya Mombasa mwezi jana baada ya miaka mitatu  kwenye ndoa.

Alieleza kuwa  sababu kuu ya kuvunja ndoa yake na mwanamuziki huyo ni kuwa na msongo wa mawazo na kutelekezwa na mumewe huku akibaini  kuwa Ali Kiba hatekelezi majukumu kama mume.

Wawili hao walioana mwaka wa 2018, chini ya kanuni za Kiislamu ambapo waliandaa sherehe kubwa mjini Mombasa huku mashabiki wakitaja harusi hiyo kuwa ya kupigiwa mfano.

Baadhi ya mashabiki waliuliza kwa nini wanandoa waoane kisha waamue kupeana talaka, huku baadhi yao wakisema kwamba wanawake wanamazoea ya kuwekelea waume zao endpo ndoa yao imevunjika.

Hizi hapa baadhi ya hisia za wanamitandao;

Isha Tachez: Gidi ako huku wajilete msisahau pia Gost ako atawachekelea kwanza kukushindikana wamtafte Bi Msafari kule Citizen

Stephen MwaniaLadies:  when their marriages goes wrong they blame man power ,when do you blame your self

Emmanuel Otieno: Wataka kuolewa na msanii,so called celebrities huku una moyo wa plastic basi utaumia sana.Waachie wenye nyoyo za chuma kufanya hivo

Julius Sifuna: Alikiba Mara Yuko na concerts Afrika na Ulaya, hiyo majumu ya kiume atatekeleza saa ngapi?? atafute Samantha atumie,nkt!

George Kelvin Simba: Walioana kwa Siri lakini wanaachana hadharani