'Sina 'beef' na Amberay,' Vera Sidika afichua

Muhtasari
  • Hatimaye Vera Sidika amejibu uvumi kwamba yeye na Amber Ray wamekuwa na ugomvi kwa muda mrefu zaidi
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Hatimaye Vera Sidika amejibu uvumi kwamba yeye na Amber Ray wamekuwa na ugomvi kwa muda mrefu zaidi.

Mama wa mtoto mmoja ambaye amewashirikisha wafuasi wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram ambapo amefichua mipango yake ya kuongeza watoto zaidi na lini hasa atapata mtoto mwingine na hata kufichua kuwa ana umri wa miaka 32 amekanushauvumi huo ambao umekuwa ukienea kwa muda mrefu.

Alionekana kwenye sehemu ya kipindi cha maswali na majibu na mashabiki wake Vera alimjibu shabiki aliyeuliza ikiwa ana ugomvi na Amber

Hapana, kwa nini, ukweli ni kuwa sina ugomvi na mtu yeyote mimi ni mtu wa aina ya kupenda kila wakati."

Kulikuwa na tetesi kwamba Amber alikuwa na uhusiano na mume wa sasa wa Vera kabla ya wawili hao kukutana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera amedai kuwa kuvunjika kwa mahusiano hakujawahi kumzuia kujitosa kwenye mahusiano mapya.

"Sijawahi kuogopa kupenda tena. Maisha yanasonga mbele na kuwa bora tu," Vera alisema alipokuwa anashirikisha mashabiki wake katika kipindi  cha maswali na majibu.