'Wanataka kukutumia,'Jimal asema ni vigumu kupata mapenzi ya kweli siku hizi

Muhtasari
  • Jimal asema ni vigumu kupata mapenzi ya kweli siku hizi
  • Jimal alikua mwanamume mseja miezi michache iliyopita, baada ya wake zake wawili kumuacha

Mfanyabiashara tajiri nchini Kenya, Jimal Marlow almaarufu Jimal Rohosafi kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram alidai kuwa ni vigumu kupata mpenzi wa dhati siku hizi, wiki chache baada ya kutangaza kuwa yuko 'single'.

Jimal alikua mwanamume mseja miezi michache iliyopita, baada ya wake zake wawili kumuacha. 

Mkewe wa kwanza Amira alikuwa wa kwanza kumwacha, baada ya kujaza talaka kwa sababu ya kutomheshimu.

Akikatisha ndoa yake ya zaidi ya miaka kumi na tano na Jimal, Amira alifichua kwamba alikuwa amechoshwa na ukosefu wake wa heshima, na akachagua kuendelea.

Kisha Jimal aliachwa na mke wake wa pili Amber Ray. Sababu kuu iliyomfanya Jimal kutengana na Amber Ray bado haijafahamika, kwani wawili hao hawajawahi kulitolea ufafanuzi suala hilo.

Amber hata hivyo tayari ameendelea na maisha yake na anaonekana mwenye furaha.

JImal mapema mwezi jana alisema kwamba anataka kuwa 'Single' ili kuzingatia biashara yake.

"Wakati mtu anasema anakupenda jua silimia 95 anataka kukutumia, ni ngumu sana kmpata mtu wa kweli," Aliandika Jimal.