Muombeeni!Mtangazaji Lion alazwa hospitali Mbusi athibitisha anaendelea vyema

Muhtasari
  • Lion amelazwa hospitali na habari za kulazwa kwake zilithibitishwa na mtangazaji mwenzake Mbusi
Mbusi na Lion

Mtangazaji wa Radiojambo Lion anafahamika kwa utangazaji wake na bidii ya kazi yake,kwa muda sasa mtangazaji huyo amekuwa akikosekana kwa kipindi cha Experience ya  Mbusi na Lion.

Lion amelazwa hospitali na habari za kulazwa kwake zilithibitishwa na mtangazaji mwenzake Mbusi.

Akizungumza na Radiojambo Mbusi alisema kwamba Lion alilazwa hospitali siku ya Ijumaa baada ya kupatikana na upungufu wa damu yaani kwa ligha ya kimombo 'Anaemia'.

Kulingana na Mbusi amelazwa katika hospitali ya Komarock Modern, Utawala kaunti ya Nairobi.

"Lion alilazwa hospitali siku ya Ijumaa baada ya kupatikana na upungufu wa damu, lakini kwa sasa anaendelea kupokea matibabu na anaendelea vyema,"Mbusi Alisema.