Sandra Dacha awashukuru mashabiki na wacheshi wenzake kwa kusimama na Akuku Danger

Muhtasari
  • Sandra Dacha awashukuru mashabiki na wacheshi wenzake kwa kusimama na Akuku Danger
Sandra Dacha almaarufu kama Silprosa na mpenzi wake Akuku Danger
Sandra Dacha almaarufu kama Silprosa na mpenzi wake Akuku Danger
Image: INSTAGRAM// SANDRA DACHA

Muigizaji Sandra Dacha ametumia akaunti yake ya Instagram na kuwashukuru Wakenya kwa moyo wote kusimama na mpenzi wake Akuku Danger, baada ya kuchangisha kiasi kikubwa cha pesa ili kulipa bili ya hospitali.

Sandra aliunda nambari ya malipo kwa mara ya kwanza kwa uchangishaji pesa wa Akuku Danger mwaka jana mnamo Desemba, baada ya kukimbizwa ICU.

Ugonjwa wa Akuku ulimfanya akae hospitalini kwa zaidi ya miezi miwili, huku madaktari wakijaribu kuokoa maisha yake.

Akuku Danger aliruhusiwa kutoka hospitalini mwezi mmoja uliopita, lakini alikuwa na takriban bili Milioni 4.5 ya hospitali ambayo ilikuwa inasubiri.

Siku ya Jumamosi wakiongozwa na Sandra Dacha, wachekeshaji wote wa Kenya walikusanyika na kutumbuiza katika ukumbi wa  Nairobi Cinema, kusaidia katika uchangishaji fedha.

Sandra Dacha amewashukuru wananchi kwa kusimama nao, huku akizidi kufichua kuwa wamekusanya Milioni 3.5 kati ya milioni 4.5 ambazo zilihitajika na Hospitali.

Zaidi ya yote alimshukuru Mwalimu Churchill kwa kusimama nao kuanzia siku ya kwanza.