Nilikuwa naishi maisha bandia -Sarah Kabu afunguka kuhusu ndoa yake

Muhtasari
  • Sarah alisema kwamba katika miaka 10 iliyopita, alikuwa na matatizo katika ndoa yake lakini mara nyingi, walisuluhisha masuala hayo faraghani

Mwanabiashara Sarah Kabu kwa mara ya kwanza amezungumzia ndoa yake yenye matatizo na mumewe wa miaka 12, Simon Kabu.

Akizungumza katika mahojiano na Christina Lewis The Voice Of East Africa, mama huyo wa watoto wawili alizungumza waziwazi kuhusu kuishi maisha ya uwongo kwa mashabiki wake.

Sarah alisema kwamba katika miaka 10 iliyopita, alikuwa na matatizo katika ndoa yake lakini mara nyingi, walisuluhisha masuala hayo faraghani.

"Asilimia 70 ya maisha ya ndoa yangu na Simon yamekuwa ya furaha na tumekuwa na wakati wetu mzuri. Pia tumekuwa na nyakati zetu mbaya ambazo hatuonyeshi watu

Nilifika mahali nikasema imetosha kwani baadhi ya watu waliniangalia, walitiwa moyo na simulizi yetu ya mtandaoni lakini nilitamani niwe na maisha ya unyenyekevu yenye upendo na amani ya moyo," Alizungumza.

Sarah aliongeza kuwa hataki kuishi maisha bandia tena.

“Nilipitia mambo mengi katika ndoa yangu na hatimaye nikaamua kuwa nitaishi maisha yangu halisi

Watu walikuwa wanahamasika sana na hadithi yetu na nilikuwa kama ninaonyesha sehemu nzuri ya maisha yangu na sio unaona sehemu mbaya. Watu wanatuangalia kama watu laini na tumekuwa shabaha laini kwa watu wabaya. ndiyo maana wakati mwingine, mimi hufanya mambo yenye utata ili watu waone tuna changamoto."