Sharti la kwanza kuchumbiana na Mnigeria ni kuwa na ‘nyash’ – Vera Sidika ashauri warembo

“Nikiwa kijijini nilikuwa nafikiria niko mnono, hivyo nilikuwa navaa nguo kubwa kubwa kuficha ‘nyash’ yangu lakini kufika Nairobi, kila mtu alikuwa anavutiwa na ‘nyash’ yangu. Ndipo nikagundua kumbe nilikuwa nakatia kitu fulani."

Muhtasari

•  "Nahisi watu walinifanya kugundua kwamba naweza tumia chenye nimebarikiwa nacho ili kupata chenye nataka," Vera Sidika alisema.

Vera Sidika.
Vera Sidika.
Image: Facebook

Mwanasosholaiti na mjasiriamali wa bidhaa za urembo, Vera Sidika amedokeza kwamba kwa sasa yuko kweye uhusiano mguu mmoja ndani na muu mwingine nje.

Akizungumza na Kalondu wa Mpasho, Sidika alisema kwamba kwa sasa anazingatia Zaidi katika kujikuza na kujivinjari mwenyewe kwa ziara ainati kote duniani, hivyo hataki kuwa katika uhusiano wa kuwajibika kwa asilimia 100.

Vera Sidika alisema kwamba anachojivunia mwaka huu ni kwamba yuko single na pia hana mimba, lakini akadokeza kwamba anatoka kimapenzi na raia wa Nigeria katika uhusiano ambao si wa kutiliwa maanani kihivyo.

“Hakuna uhusiano rasmi kwa sababu kwangu, sitaki kitu chochote cha kuwajibikia kwa sasa, ninataka tu kujivinjari. Ni kweli ninatoka kimapenzi na mtu Fulani lakini siwezi sema kwamba niko kwenye uhusiano. Niko 50-50; mguu mmoja ndani na mguu mwingine nje,” Sidika alisema.

Mama huyo wa watoto wawili alifichua kwamba anachumbiana na raia wa Nigeria akidadavua baadhi ya ujanja kwa warembo ambao wana uchu wa kuchumbiana na raia wa taifa hilo la Afrika Magharibi ambao wanapigiwa saluti kwa weledi wao katika mapenzi.

“Si Mkenya, ni Mnigeria, wale ndio wanajua kabisa. Wanasema ukishaamua kwenda Nigeria hurudi, ni kama mimi nilikuwa nimepotea kisha nikajitambua. Ananitunza vizuri sana. Sharti la kwanza kama unataka kuchumbiana na Mnigeria, kuwa na ‘nyash’. Hata hivyo simaanishi kwamba kila Mnigeria anapenda ‘Nyash’ lakini unajua kama mrembo ni lazima uwe nayo,” Vera Sidika alimwambia Kalondu.

Sidika ambaye alijizolea umaarufu kutokana na umbile lake la kiuno pana alisema kwamba alikuwa anafikiria ni aibu na kuvaa mavazi ya kumpwerepweta lakini baada ya kufika Nairobi, akagundua kwamba anakalia kitu ambacho angekitumia vizuri kingemfaidi.

“Nikiwa kijijini nilikuwa nafikiria niko mnono, hivyo nilikuwa navaa nguo kubwa kubwa kuficha ‘nyash’ yangu lakini kufika Nairobi, kila mtu alikuwa anavutiwa na ‘nyash’ yangu. Ndipo nikagundua kumbe nilikuwa nakatia kitu fulani. Nahisi watu walinifanya kugundua kwamba naweza tumia chenye nimebarikiwa nacho ili kupata chenye nataka, na hakuna jambo lolote baya kuhusu hilo,” Vera Sidika alisema kwa kujitapa.