Vera anyoosha maelezo kuhusu uvumi wa kurudiana na Brown Mauzo kisa kufanana kwa tattoo

Sidika na Mauzo waliachana Septemba mwaka jana na Katika kipindi chao cha uchumba, Sidika na Mauzo walifanikiwa kupata watoto wawili, binti na mvulana ambao wote kwa sasa wanalelewa na mama yao.

VERA SIDIKA.
VERA SIDIKA.
Image: Instagram

Mjasiriamali na mwanasosholaiti Vera Sidika amekanisha uvumi wa kurudiana na baba watoto wake, Brown Mauzo.

Uvumi huo uliibuliwa na sehemu ya mashabiki wake ambao wako makini katika kila kitu wakati bintiye Vera, Asia Brown alionekana kwenye bega lake.

Hata hivyo, katika bega hilo, Vera Sidika alionekana kuwa na tattoo moja kubwa ambayo inashabihiana na tattoo katika mwili wa Brown Mauzo.

Shabiki mmoja alishindwa kukimya na kumuuliza moja kwa moja, akihoji kwamba tattoo hiyo haikuwa ngeni kwa wengi kwani Brown Mauzo mara nyingi huionyesha akipiga picha zake na fulana tu.

Sidika, ambaye alionekana kukerwa na hilo alisema kwamba tattoo hiyo imekuwa kwenye mwili wake kwa muda mrefu na kuwataka wanaoendesha uvumi kwamba amerudiana na ex wake kukoma.

“Huh, kwani nyinyi watu hamjui tattoo kwenye mkono wangu? Mnamaanisha nyinyi wote hamjui hii tattoo?” Sidika aliuliza huku akionyesha mwili wake kwa ukamilifu na sio bega tu.

Alikwenda mbele na kufafanua kwamba hana mpango wowote wa kurudiana na ex wake na hilo halitotokea wakati wowote hivi karibuni.

“Tafadhali acha nieleweke hivi, sijarudiana na ex wangu wala sifikirii kurudiana naye. Hilo halitotokea, kwa hiyo tafadhali acha huo uvumi na matarajio, ahsante,” Vera Sidika alisema kupitia instastory yake.

Sidika ba Mauzo waliweka wazi kutengana mwezi Septemba mwaka jana baada ya kuchumbiana kwa takribani miaka mitatu.

Katika kipindi chao cha uchumba, Sidika na Mauzo walifanikiwa kupata watoto wawili, binti na mvulana ambao wote kwa sasa wanalelewa na mama yao.