Zari awezwa na hisia baada ya mchoraji kumkabidhi picha ya marehemu mamake

Muhtasari

•Zari alipokea picha hiyo katika hoteli ambapo alikutana na mashabiki wake kutoka hapa nchini Kenya.

•Zari  alisema kwa kawaida huwa hapendi suprise lakini  siku hiyo alishawishika kukubali.

Zari akipokea picha ya mamake marehemu.
Zari akipokea picha ya mamake marehemu.
Image: Instagram

Zari Hassan alijawa na hisia baada ya mchoraji kumkabidhi  picha ya marehemu mamake wakati wa ziara yake ya Kenya.

Mama huyo wa watoto watano alisisimuliwa na kitendo cha mchoraji huyo na kudondokwa na machozi  baada ya kuipokea picha hiyo iliyokuwa imechorwa kwa kalamu nyeusi.

Zari alipokea picha hiyo katika hoteli ambapo alikutana na mashabiki wake kutoka hapa nchini Kenya.

'Nilitarajia kushangazwa na Maua wala si picha ya mama yangu'  Zari alisema.

Mchoraji huyo mwenye talanta kubwa alipongezwa na Zari kwa kazi yake ya usanii inayovutia sana.

''Hii ndiyo picha napenda zaidi '' Zari alisema

Mke huyo wa zamani wa Diamond  alisema kwa kawaida huwa hapendi suprise lakini  siku hiyo alishawishika kukubali.

Wakati huo huo, Zari pia alipokea picha ya mtoto wake kutoka kwa  mchoraji  mwingine ambaye pia kazi yake yalikuwa sawa.

''Nawashukuru kwa kugusa maisha yangu kwa njia tofauti nyinyi ni wa ajabu'' Zari alisema.

Mamake Zari, Bi Halima Hassan alifariki  mwaka wa 2017 kutokana na matatizo ya moyo, hali iliyomfanya  kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha hospitali ya Nakasero

Wakati wa ziara yake Nairobi, Zari alipata nafasi ya kufanya  kazi na makampuni mbalimbali na inadaiwa madhumuni yake makuu yalikuwa ya kufanya kazi na  kampuni ya Fine Urban.