H.Baba adai malipo katika wimbo 'Attitude'

kibao hicho kilishirikisha Mastaa Harmonize, H.baba na Awilo Longomba

Muhtasari

•Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hamisi Ramadhani Baba maarufu kama 'H.Baba' kutoka Bongo akihojiwa na runinga ya Top level Tz  alisema kuwa Harmonize ako na deni yake mingi.

•Staa huyo  ambaye alishirikisha Harmonize na Staa wa CONGO Awilo Longomba kwa ngoma yao ya 'Attitude', alikiri kwamba hajapata hela zilizotakana  kazi hiyo walioifanya. 

H.Baba
H.Baba
Image: HISANI

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hamisi Ramadhani Baba maarufu kama 'H.Baba' kutoka Bongo akihojiwa na runinga ya Top level Tz  alisema kuwa Harmonize ako na deni yake mingi.

Staa huyo  ambaye alishirikisha Harmonize na Staa wa Congo Awilo Longomba kwa ngoma yao ya 'Attitude', alikiri kwamba hajapata hela zilizotakana  na kazi hiyo walioifanya. 

''Mimi sipendi uongo, na nitasema ukweli leo,we unajua nilivyo pambana na wewe kutengeneza wimbo 'Attitude' na haujanilipa chochote, mimi sitaki kulipwa kwa yale yote nilikuwa nayafanya, bali nataka kulipwa kwa kazi niliyoyafanya ya ngoma ya 'Attitude' hiyo tu'' H.Baba alisema.

H.Baba pia aliongeza kwa kusema kuwa Harmonize ni mtu mwenye ukabila,kitu ambacho aliwai mdokezia kuwa kitamsababishia matatizo.

''Mle ndani asilimia kubwa, wengi ni wa kabila lake, nikamwambia kuwa hiyo sio mzuri changanya watu,hawa watoke huku wale watoke pale, wakaja Kil na Chidi na Angela, wanafanya vizuri kwa usani, lakini watu bado wanahisi kuwa kuna ukabila'' H.Baba alisema.

Staa huyo, aliweka wazi kuwa Harmonize hana heshima kwa wasanii waliomtangulia kwenye gemu ya muziki, na ata wale waliomsadia hawezi kuwaomba msamaha pindi alipowakosea.

''Kama unasema ulikuwa kijijini na kutazama H.Baba kwa Tv wewe  na wazazi wako alafu mnafurahia, usije ukanidhulumu leo,anasimulia viti ambavyo mimi mwenyewe nilishasahau, sisi leo  wasanii wa zamani tunasemwa vibaya,ooh mara hawana kitu, hawana lolote,ooh wamefilisika, msitusema hivyo maanake sisi pia tunaupitia hali gumu'' H.Baba alisema.

H.Baba pia alisema kuwa Harmonize hajui kuomba msamaha kwa wanaume wenzake aliyewakosea kama Diamond, lakini ako mwepesi wakuomba mwanamke msamaha

''Wanawake unawapigia simu na kusema,halo baby nisamehe, unajua nilikukosea, naomba tu unisamehe nina zawadi yako hapa, lakini mwanaume ambaye ulikosana naye unasema kuwa hutaki kusameheana naye, msamaha umeumbiwa pande zote mbili,mwanaume na mwanamke, kwa nini we kila siku masamaha wako ni kwa wanawake tu'' H.Baba alisema.