Rayvanny ananunua gari la Ksh1.5M na kuliteketeza

Aliamua kufanya video hiyo kuwa halisi kabisa kwa kuliteketeza gari aina ya Toyota Altezza

Muhtasari

• Mwimbaji mashuhuri wa Tanzania Rayvanny haheshi vituko, kwa mara nyingine aliwashangaza wengi baada ya kununua gari aina ya Toyota Altezza na kuliteketeza makusudi.

• Aliamua kufanya video hiyo kuwa halisi kabisa kwa kuliteketeza gari aina ya Toyota Altezza.

Msanii Rayvanny na picha ya gari alilochoma wakati wa kufanya video
Image: Rayvanny(Instagram screenshot)

Mwimbaji mashuhuri wa Tanzania Rayvanny haheshi vituko, kwa mara nyingine aliwashangaza wengi baada ya kununua gari aina ya Toyota Altezza na kuliteketeza makusudi.

Staa huyo wa Bongo alipata gari aina ya Toyota Altezza ambalo bei yake ni kati ya Ksh. 670,000 na shilingi milioni 1.5  na kuliteketeza kwa ajili ya kurekodi video yake mpya ya muziki.

Rayvanny anarekodi video mpya ya kibao 'Te Quiero' akiwa amemshirikisha Marioo. Aliamua kufanya video hiyo kuwa halisi kabisa akiteketeza gari.

"Najua kweli ni uhalisia lakini yani hakuna scene imeniumiza moyo kama scene ya kuchoma gari. Director naomba tuishie hapa kuchoma choma vitu'' Rayvanny alisema.

Uamuzi wa Rayvanny kuchoma moto gari jipya alilonunua Toyota Altezza umekuja wiki chache baada ya kuteketeza kwa makusudi nyumba yake mpya aliyoijenga.

Muimbaji huyo wa Bongo Fleva aliteketeza jumba lake la kifahari kwa lengo moja tu la kushoot video ya wimbo wake mpya ‘I Miss You’ aliomshirikisha Zuchu.

Vanny Boy alijigamba kuwa video ya 'I Miss You' ndiyo video ya muziki ghali zaidi kuwahi kushutiwa nchini kwao Tanzania.

Alisema zaidi kwamba alijenga nyumba hiyo mpya kutoka mwanzo na kuichoma moto kwa makusudi kwa ajili ya tukio la video mpya ya muziki.