Mtangazaji Joey Muthengi alazwa hospitalini

Muthengi hata hivyo bado hajafichua ugonjwa uliomshambulia

Muhtasari

• Kwa sasa Joey anatangaza kwenye show ya asubuhi ya Power Breakfast akiwa na Willis Raburu na Fred Indimuli.

Mtangazaji Joey Muthengi alazwa hospitalini
Mtangazaji Joey Muthengi alazwa hospitalini
Image: Joey Muthengi//Instagram

Mtangazaji wa zamani wa stesheni ya Citizen TV Joey Muthengi amelazwa hospitalini kwa siku mbili sasa.

Muthengi hata hivyo bado hajafichua ugonjwa uliomshambulia hadi kusababisha kulazwa kwake. Pia hajafichua hospitali ambayo amelazwa.

Alitangaza habari za kulazwa kwake kupitia mitandao ya kijamii ambako alipakia picha ya exray na kueleza jinsi anavyotamani kutoka nje tena.

“Hapa pamekuwa nyumbani kwa siku mbili zilizopita,”alisema.

Mtangazaji huyu  alijipatia umaarufu baada ya kuwa mtangazaji wa redio katika Capital FM kuanzia 2009 hadi 2013.

Baadaye Joey aiweza kuwa mtangazaji wa shoo ya 10/10 kwenye Citizen TV akishirikiana na Willis Raburu kama mtangazaji mwenza mwaka wa 2016 mpaka Novemba 2018.

Mtangazaji alipoiwacha kazi yake alidhihirisha mambo hayakuwa shwari vile kwa muda na alipotea kwenye mtandao kwa muda.

Kwa sasa Joey anatangaza kwenye show ya asubuhi ya Power Breakfast akiwa na Willis Raburu na Fred Indimuli.

Joey aliweza kuanzisha Wakfu inayoitwa 'Muthengi Foundation' mwaka 2014 akiwa na mwanamuziki David Muthengi alimaarufu Holy Dave.

Wakfu huo ina nia ya kuwatolea familia zisizojiweza chakula ili wawe na kitu cha kuweka mezani.

Joey pia alitaka kuwapa msaada watoto wasio na karo ama vitabu.

Joey bado hajaweza kutangaza uhusiano wake wa kimapenzi na kwa sasa mpenzi wake hajatambulika.

Miezi tisa iliyopita, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Joey alijibu swali ambalo mashabiki wake wengi waliendelea kuuliza kuhusu kuolewa kwake.

Alifichua kwa ujasiri kwamba hajaolewa na ikiwa alikuwa ameolewa, anaweza kuwa akimpakia mumewe mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii.

“Sijaolewa…unafikiri ningekuwa nimeolewa halafu ninamficha mume mzima kwenye mitandao ya kijamii ya instagram

Kama nilikuwa nimeolewa nitakuwa najivunia sana huyo mwanaume na atakuwa kwenye page yangu, mimi nitakuwa mmoja kati ya watu ambao mnakerwa nao, utakuwa kama huyu kifaranga anaweza kuacha kumpost mume wake, hakika sijaolewa,” alisema Joey Muthengi.

Hadi sasa hajaweza kufichua uhusiano wake.