Nimetimiza ndoto zangu-Thee Pluto baada ya kubarikiwa na mtoto wa kike

Muhtasari
  • Aliendelea na kumshukuru mwanawe, kwa kumbadilisha na kufanya aitwe baba,na kupewa heshima
  • Awali alimwandikia mpenzi wake ujumbe mtamu kabla ya kujifungua
Thee Pluto,Mwanawe na Felicity
Image: FELICITYINSTAGRAM

Mwanavlogu Thee Pluto amedokeza kuwa ametimiza ndoto zake baada ya kubarikiwa na mtoto wa kike.

Mwanavlogu huyo alifichua kwamba mwanawe alizaliwa siku ya Ijumaa.

Aliendelea na kumshukuru mwanawe, kwa kumbadilisha na kufanya aitwe baba,na kupewa heshima.

"Nimetimiza ndoto zangu kwa kumpata mwanangu. Karibu duniani mtoto wangu @zoey_pluto Umenibadilishia jina nikawa mzazi na ukanipa heshima. Nakuombea Maisha mema. My true love ❤️,"Aliandika Pluto.

Awali alimwandikia mpenzi wake ujumbe mtamu kabla ya kujifungua.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Pluto alipakia picha yake na Felicity wakiwa hospitalini wakiijitayarisha kujifungua kwa mama huyo.

“Wakati unadidimia. Wacha nianze kwa kusema kuwa kwangu wewe ni superhero. Mtu aliye na nguvu na upendo wangu kwako unakua kila siku. Umekuwa mrembo zaidi ya nyakati zote,” Pluto alisema.

Hata hivyo Pluto alisema kuwa atafanya anachoweza ili mtoto na mpenzi wake wapate mahitaji yao na upendo kamili.

“Nina hofu kwa kinachokuja. Nina wasiwasi ya kuwa mtoto wetu hatanipenda ama kushindwa kutekeleza wajibu wangu vizuri, ya kuwa wanaweza kukukasirisha kisha kubadilisha mahaba ambayo tulikuwa nayo. Lakini wakati wowote ambao nina mawazo haya, nakuangalia tu kisha ninakumbuka jinsi ulivyotatua chochote ambacho kimekuwa kikikukwana wakati huu wa ujauzito,” mwanavlogu huyo alisema.