Diana Marua asherehekea miaka 7 ya ndoa na Bahati

Bahati alibainisha kuwa maisha yake yalikamilika wakati ambapo alimpata mke huyo wake .

Muhtasari

•Katika chapisho la Instagram, mama huyo wa watoto watatu alionyesha fahari yake kuona jinsi wanavyofanana sana.

•Mwanavlogu huyo alidokeza kuwa mapenzi yake na mwimbaji huyo wa zamani wa injili ni ya kweli na ya kujivunia.

Diana Marua na Bahati
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mwanavlogu na rapa mashuhuri Diana Marua amesherehekea miaka saba ya kuwa pamoja na mwimbaji Kelvin Kioko almaarufu Bahati.

Katika chapisho la Instagram, mama huyo wa watoto watatu alionyesha fahari yake kuona jinsi wanavyofanana sana.

Alibainisha kuwa yeye na Bahati wanafanana sio kimuonekano tu bali pia, kimavazi na hata lugha yao ni sawa.

"Miaka 7 ambayo imepita, tunafanana 😂, tunaongea lugha moja, vicheko vyetu ni vinafanana na tangu wakati wote hatujawahi kuacha kufananisha mavazi yetu 💃," aliandika chini ya picha zake na mumewe wakiwa na mavazi sawa.

Mwanavlogu huyo alidokeza kuwa mapenzi yake na mwimbaji huyo wa zamani wa injili ni ya kweli na ya kujivunia.

Bahati kwa upande wake alibainisha kuwa maisha yake yalikamilika wakati ambapo alimpata mke huyo wake na kuweka wazi kuwa amemtosha.

"Nilipokupata, nilipata nusu yangu bora na unatosha Diana Marua," alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Bahati alimtambulisha Diana kama 'mshirika wake wa maombi' takriban miaka sita iliyopita kabla ya kubainika kuwa wanachumbiana.

Wawili hao wamekuwa wakiishi pamoja katika ndoa na tayari wamebarikiwa na watoto watatu pamoja. Pia wanalea mtoto mwingine mmoja, Morgan Bahati ambay Bahati alitoa kwenye chumba cha watoto.

Mwaka jana, Bahati alifunguka kuhusu mipango ya kufunga pingu za maisha na Diana Marua hivi karibuni.

Katika sherehe ya kufichua jinsia ya mtoto, mwanamuziki huyo alisema kuwa anapanga harusi kubwa ya kifahari.

Alisema sababu ya kukawia kufanya harusi licha ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu ni kwa kuwa hangetaka kufanya harusi ndogo.

"Unajua mimi ni mtu anayependa kufanya mambo kwa kuongeza ladha, nikiandaa hafla napenda kuandaa hafla kubwa," alisema.

Kabla ya kujitosa kwenye mahusiano na Diana Marua, mwimbaji huyo alikuwa akichumbiana na Yvette Obura ambaye ana binti mmoja naye.