Ni muziki wa Uganda ndio ulionifanya kuwa mwanamuziki niliye leo- Bien Aime Baraza

"Sana sana ilikuwa muziki wa Uganda ndio ulinifanya kuwa mwanamuziki niliye leo"

Muhtasari
  • Bien alisifu nchi ya Uganda na kukubli kuwa wanamuziki mashuhuri kutoka nchi hiyo walimfanya kupaa kimuziki na anawashukuru sana.
  • "Ntaimba nyimbo nzuri sana kutoka kwa msanii mashuhuri, mtu amabye hunipea motisha sana kama msanii. Wimbo ni Valu Valu kutoka kwa Jose Chameleon".
Bien
Bien
Image: Hisani

Mwanamuziki wa Kenya anayejulikana kama Bien-Aime Baraza amefichua kuwa muziki wa Uganda ndio uliomfanya kuwa msanii aliye leo.

Bien alisifu nchi ya Uganda na kukubli kuwa wanamuziki mashuhuri kutoka nchi hiyo walimfanya kupaa kimuziki na anawashukuru sana.

"Sana sana ilikuwa muziki wa Uganda ndio ulinifanya kuwa mwanamuziki niliye leo", Bien  alisema kwa tamasha ambayo iliyopewa jina "A Night With Bien" iliyofanyika Kampala Hoteli wa Serena.

Aliendeleza kueleza upendo wake mkubwa kwa nchi hiyo na kuwashukuru kwa michango yao na kuiweka Afrika kwenye ramani.

"Nashukuru  kwa uwepo wenu kama nchi na kama watu, na kile mulichofanya kwa bara. Nawapenda", Bien alisema. 

Wakati wa tamasha lake, aliweza kuimba wimbo wa kiganda kuonyesha upendo alionao kwa nchi hiyo. wimboaliyoimba ni "Mbozi Za'malwa"  ambayo ni wimbo yao (Sauti sol) wakimshiriki Bebe Cool.

Katika mohajiano na radio ya Uganda Jumatano Februari 14 kabla ya tamasha yake, alisema kuwa mwanamuziki anayejulikana kama Jose Chameleon wa Uganda ambaye humtia motisha  sana. Pia aliweza  kuimba wimbo wa Jose inayojulikana kama "Valu Valu".

"Ntaimba nyimbo nzuri sana kutoka kwa msanii mashuhuri, mtu amabye hunipea motisha sana kama msanii. Wimbo ni Valu Valu kutoka kwa Jose Chameleon".

Bien ameo mshabiki wa dansi Chikwere anayejulikana kama Chiki Kuruka. Chiki anataoka nchi ya Uganda.