Bien Sol ataja sababu ya kuchukia githeri,kupiga marufuku mapishi yake nyumbani kwake

Pia aliweka wazi kwamba anachukia kabichi.

Muhtasari

• Bien aliwashangaza wengi aliposema kwamba anachukia githeri kiasi kwamba alipiga mapisho yake marufuku katika jiko lake.

Bien achukia githeri.
Bien achukia githeri.
Image: Facebook, Maktaba

Msanii Bien Aime Baraza ambaye ni kiongozi wa bendi ya muda mrefu yenye mafanikio makubwa kutoka humu nchini Sauti Sol amefichua kwa nini anachukia msosi wa pure.

Pure ni mchanganyiko wa mahindi na maharagwe yaliyochemshwa kwa lugha nyepesi wengi wanafahamu chakula hicho kama ‘Githeri’.

Msanii huyo hivi majuzi aliketi kwenye kiti cha mazungumzo na podikasti moja na aliweza kuulizwa baadhi ya mswali ya kibinafsi ikiwemo vyakula ambavyo anavikubali na vile anavyovichukia.

Katika kipande cha video ambacho alipakia kwenye Instastory yake na abacho kimeenezwa mitandaoni, alikuwa anajibu kuhusu chakula ambacho anakichukia Zaidi katika maisha yake.

Bien aliwashangaza wengi aliposema kwamba anachukia githeri kiasi kwamba alipiga mapisho yake marufuku katika jiko lake.

“Githeri, mchanganyiko wa mahindi na maharagwe. Nakichukia sana chakula hicho, siwezi kivumilia katika nyumba yangu. Nyumbani nilishamwaambia mfanyikazi wangu wa ndani, mamangu anajua na hata mke wangu anajua kuwa hakuna mtu anayekubaliwa kupika chakula cha aina hiyo katika jiko langu,” Bien alisema.

Kisha jopo liliuliza ikiwa Bien alijaribu kuongeza viritubishi kwenye msosi wake wa githeri.

Alihusisha chuki yake na chakula hicho pendwa na Wakenya wengi wenye maisha ya kipato cha chini haswa majira ya mchana kwenye maeneo ya kazini na enzi za masomo yake katika shule ya bweni.

Pia aliweka wazi kwamba anachukia kabichi.

"Nilijaribu kula na parachichi, BlueBand na vitu vingine, lakini haikufanya kazi. Pia situmii kabichi kwa sababu ya shule ya upili." Mwimbaji huyo alisema kwa madaha.