Washukiwa 6 wa mauaji ya rapa AKA wa Afrika Kusini wakamatwa

Watu sita wamekamatwa na kuzuiliwa kuhusiana na mauaji wa rapa wa Afrika Kusini Kiernan Jarryd Forbes, almaarufu AKA.

Muhtasari
  • Sita hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Alhamisi idara ya polisi ilisema. 
Familia ya AKA yamkabidhi tuzo zake 4 kwenye kaburi lake.
Familia ya AKA yamkabidhi tuzo zake 4 kwenye kaburi lake.
Image: Twitter

Watu sita wamekamatwa na kuzuiliwa kuhusiana na mauaji wa rapa wa Afrika Kusini Kiernan Jarryd Forbes, almaarufu AKA na meneja na wake wa zamani, Tebello “Tibz” Motsoane , Waziri wa Polisi wa Afrika Kusini Bheki Cele alisema Jumanne usiku.

Washukiwa hao sita wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Alhamisi, alisema Cele katika mkutano na waandishi wa habari  katika makao makuu ya Huduma ya Polisi mjini Durban.

Cele aliungana na mkuu wa mkoa wa KZN, Luteni Jenerali Nhlanhla Mkhwanazi na Kamishna wa Polisi wa Kitaifa Luteni Jenerali Fannie Masemola.

AKA (35) na Motsoane waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye Barabara ya Florida huko Morningside, Durban, tarehe 10 Februari 2023.

Tukio hilo lilifanyika nje ya mgahawa wa Wish Florida. Polisi walisema AKA na Motsoane walikuwa wakielekea kwenye gari lao walipofikiwa na watu wawili wenye silaha ambao walivuka barabara na kuwafyatulia risasi.

"Washukiwa hawa sita walicheza majukumu tofauti wakati wa operesheni. Tuna mratibu, ambaye kimsingi ndiye mkuu wa kila kitu. Yuko chini ya ulinzi. Tuna wapiga risasi wawili. Tuna watazamaji wawili - mmoja wa watazamaji alikuwa ndani ya mgahawa akitazama  Bw Forbes na marafiki zake - pamoja na mratibu wa bunduki na magari, kwa sababu gari lililotumika kama sehemu ya kutoroka na bunduki zilizotumiwa kupiga risasi, wote walikodiwa," Mkhwanazi alisema.

Mmoja wa watazamaji anaripotiwa kufuata Forbes kutoka uwanja wa ndege alipowasili, kwenye hoteli yake na mgahawa wa Wish Florida.

Mtu huyu pia alikuwa na jukumu la kukusanya timu ya hitmen na rasilimali, na kuwalipa "thawabu zao" kazi ilipofanywa.

Wakati wa kukamatwa askari wa polisi pia walipata magari manne, bunduki na cartridges ambayo yaichukuliwa  kutoka eneo la uhalifu ambazo zilihusishwa na eneo lingine la uhalifu ambapo risasi nyingine ilitokea.

Gari la kwanza, Mercedes-Benz,  lilipatikana mnamo 6 Machi 2023, na bunduki ambayo ilitumiwa kupiga Forbes ilipatikana mnamo 22 Aprili.

AKA alikuwa mshindi wa tuzo, msanii wa muziki wa hip-hop wa Afrika Kusini aliyetambulika kimataifa akiwa na albamu kadhaa zilizosifiwa chini ya ukanda wake.