Binti wa marehemu AKA awanyanyua na kuwaliza watu kwa kuimba wimbo wa babake (Video)

Baada ya kupokea tuzo ya wimbo ulioshinda, binti wa AKA alichukuwa maikrofoni na kuwataka umati waimbe pamoje naye, wengi walionekana kutokwa na machozi.

Muhtasari

• Baada ya video hiyo kusambaa kwenye Twitter, mashabiki hawakuweza kuipokea vya kutosha.

• Iliwakumbusha mashabiki wengi wa AKA, haswa aliposema, "Njoo, imba nami", kauli ambayo AKA alipenda kuitumia akiwa jukwaani.

Binti wa AKA awanyanyua mashabiki kwa kuimba wimbo wa babake.
Binti wa AKA awanyanyua mashabiki kwa kuimba wimbo wa babake.
Image: Twitter

Usiku wa Jumapili ulikuwa wa aina yake na wa kukumbukwa na mashabiki wa msanii marehemu AKA kutoka Afrika Kusini ambapo msanii huyo licha ya kutokuwepo kwake kwenye jukwaa la muziki kwa takribani miezi minne sasa, bado kazi zake za Sanaa zinazidi kutamba na kujinyakulia tuzo.

Katika usiku huo, matukio mbali mbali yalitokea ambapo tukio kubwa lilikuwa kutolewa kwa tuzo za muziki za Metro FM nchini Afrika Kusini.

Kando na kwamba AKA alishinda tuzo nne katika vipengele vya collabo bora ya mwaka ambapo ngoma yake na Nasty C, msanii bora wa mwaka na rapa bora lakini pia msanii bora katika kitengo cha wasanii wa kiume, pia tukio kubwa lilikuwa lile la binti yake kusimamisha umati kwa kuimba wimbo wa babake.

Wimbo wa Lemonade, ama Lemons kama unavyojulikana na wengi ndio wimbo ulioshinda tuzo ya collabo bora ya mwaka ambapo alimshirikisha msanii Nasty C na ndio wimbo ambao binti yake aliuimba kwa ustadi baada ya kupokea tuzo 4 za babake.

Kairo Forbes alipanda jukwaani na babu na bibi yake kupokea tuzo ya Wimbo Bora wa Ushirikiano wa AKA akimshirikisha Nasty C.

Walipokuwa wakienda jukwaani, binti ya AKA alionyesha kwamba alikuwa akijifunza vyema huku akiinua umati kwa kuimba kwake vizuri.

Kairo alipochukua maikrofoni, aliwaomba mashabiki waimbe pamoja naye wimbo ulioshinda tuzo ‘Limonade (lemon)’, ambao ulikuwa wa kupendeza.

Baada ya kuimba mistari michache, Kairo Forbes alitoa mtiririko kwa umati, nao walipenda, wakipiga makofi na kutabasamu.

Bila shaka, hii ni tuzo ya mwisho ya AKA ya Metro FM, lakini matumaini ni kwamba Forbes mwingine kupitia kwa binti yake ataiendeleza historia yake kimuziki.

Baada ya video hiyo kusambaa kwenye Twitter, mashabiki hawakuweza kuipokea vya kutosha. Iliwakumbusha mashabiki wengi wa AKA, haswa aliposema, "Njoo, imba nami" - kauli ambayo AKA alikuwa anapenda kuitumia sana akiwa jukwaani akitumbuiza.