Joe Mfalme avunja kimya kwa mara ya kwanza baada ya kuachiliwa kutoka jela

Wakati Mfalme alikwepa kuzungumzia maelezo ya kesi hiyo, alishughulikia uvumi wa mtafaruku kati yake na Ballo

Muhtasari
  • Aliutaja kuwa wakati wa kutafakari, bila kingine chochote cha kufanya ila “kufikiri, kustarehe, na kulala.”
DJ JOE MFALME
DJ JOE MFALME
Image: Facebook

DJ Joe Mfalme amesalia kimya tangu aachiliwe kutoka rumande  baada ya kuzuiliwa kwa siku 14 kuhusiana na mauaji ya afisa wa polisi Felix Kelian.

Mfalme aliachiliwa kwa sharti la kutoa ushahidi wake upande wa mashtaka na kusababisha baadhi ya watu kuhisi kuwa alimsaliti rafiki yake wa muda mrefu Hype Ballo ili kujiokoa.

“Watu hawajui habari kamili, na kwa kuwa suala hilo kwa sasa liko mahakamani, sitalizungumzia. Maoni ya umma hayaepukiki, lakini ninataka kuweka wazi kuwa mimi na Hype Ballo bado tuko katika uhusiano mzuri. Hata hivyo, kutokana na uchunguzi unaoendelea, haturuhusiwi kuzungumzia kisa hicho,” DJ Joe alisema.

Katika mahojiano ya hivi majuzi na Ankali Ray, Mfalme alifunguka machache kuhusu uzoefu wake jela.

Aliutaja kuwa wakati wa kutafakari, bila kingine chochote cha kufanya ila “kufikiri, kustarehe, na kulala.”

Wakati Mfalme alikwepa kuzungumzia maelezo ya kesi hiyo, alishughulikia uvumi wa mtafaruku kati yake na Ballo.

Alitupilia mbali madai haya, akisema kwamba hadithi nyingi zinazosambazwa si za kweli, na kwamba yeye na Ballo wanasalia kuwa marafiki.

 Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma katika barua yake ya Aprili 5, 2024, kushauri kuwa watano kati ya saba wawe shahidi katika kesi hiyo.

Katika barua hiyo hiyo, DPP alimshtaki mlalamikiwa wa kwanza Allan Ochieng' kwa mauaji hayo.