Trisha Khalid aweka wazi uhusiano wake na Flaqo

Trishna alishikilia kuwa uhusiano wake na Flaqo ni uhusiano wa kazi tu na sio zaidi.

Muhtasari
  • Madai hayo yaliongezeka kwa sababu ya muungano ambao wawili hao wanayo wakati wakifanya video zao za vichekesho.
Trisha Khalid na Flaqo
Image: Instagram

Muigizaji na mwanasosholaiti Trisha Khalid amenaswa katika mazungumzo kuhusu kama kuna jambo zaidi kati yake na mchekeshaji Flaqo.

Madai hayo yaliongezeka kwa sababu ya muungano ambao wawili hao wanayo wakati wakifanya video zao za vichekesho.

Wamekuwa wakifanya video kadhaa pamoja na inaonekana kama wameingiana vizuri na maudhui yao yanavutia zaidi.

Wanamtandao wamekuwa wepesi kuhitimisha kufuatia uhusiano wao.

Majibu ya Trisha kwa haya yote yalikuwa karibu. Alishiriki upande wake wa hadithi katika mahojiano ya hivi majuzi na kituo kimoja cha humu nchini; ambapo alishikilia kuwa uhusiano wake na Flaqo ni uhusiano wa kazi tu na sio zaidi.

"Mimi na Flaqo ni marafiki wazuri tu na tunarekodi maudhui. Hakuna kingine",Trisha alieleza.

Trisha alieleza zaidi kuwa tayari yuko kwenye uhusiano.

"Nina mwanaume. Siko single mimi. Nani alikuambia niko single? Mimi niko na mtu. Kaa ukijua Niko mtu na hakuna kinachoendelea kati yangu na Flaqo".

Trisha hakutoa maelezo zaidi kuhusu uhusiano wake wa sasa, akisema anapendelea kuuficha.

Mpenzi wa sasa wa Flaqo Keranta alijibu chapisho hilo akiandika;"Unajua nacheka kwanini....."