"Najua haitakuwa rahisi" Njia maalum Kareh B anapanga kumuenzi marehemu mwanawe

Marehemu Mwadulo aliaga baada ya basi lililokuwa limebeba wanafunzi wengine wa shule ya upili ya Chavakali kuanguka.

Muhtasari

•Kareh B yuko kwenye harakati za kuzindua wakfu wa Dulo Foundation, kwa heshima ya marehemu mwanawe Joseph Mwadulo.

•Alionyesha picha ya nembo ya wakfu huo ambayo inafanyiwa kazi na kuomba Mungu amsaidie anapofanya kazi ya kuanzisha wakfu huo.

Image: FACEBOOK// KAREH B

Mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za Mugithi Mary Wangari Gioche almaarufu Kareh B yuko kwenye harakati za kuzindua wakfu wa Dulo Foundation, kwa heshima ya marehemu mwanawe Joseph Mwadulo.

Marehemu Mwadulo alipoteza maisha yake mnamo Machi 31, 2024 baada ya basi lililokuwa limembeba yeye na wanafunzi wengine wa shule ya upili ya Chavakali kuanguka katika mzunguko wa Mamboleo, katika kaunti ya Kisumu. Wanafunzi hao walikuwa wakielekea nyumbani katikati mwa mapumziko ya nusu muhula wakati ajali hiyo ilipotokea.

Katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, Kareh B ameendelea kudokeza kuhusu ‘Dulo Foundation’ ambayo anasema itaangazia ustawi wa jumla kwa vijana. Pia amesema kuwa wakfu huo pia utasaidia wazazi walio na huzuni ambao wamepoteza watoto wao.

“Nafanyia kazi nembo ya #dulofoundation. Tutazingatia ustawi wa jumla kwa vijana, yaani kimwili, kiakili, kihisia, kiroho, nk. Bila kusahau wazazi, baba na mama wanaoomboleza. Najua hii haitakuwa rahisi.., " Kareh B alisema.

Mwanamuziki huyo mahiri alionyesha picha ya nembo ya wakfu huo ambayo inafanyiwa kazi. Pia alimwomba Mungu amsaidie anapofanya kazi ya kuanzisha wakfu huo.

Image: FACEBOOK// KAREH B

Haya yanajiri takriban miezi miwili baada ya mwimbaji huyo maarufu Mugithi kumpoteza mwanawe Joe Mwadulo ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya upili ya Chavakali wakati wa kifo chake. Kijana huyo alikufa akiwa na umri wa miaka 17.

Joseph Mwadulo, mwana wa mwimbaji Mugiithi KarehB alizikwa, nyumbani kwa mzazi wake huko Kimangaru, Kaunti ya Embu mnamo Aprili 12.

Mwadulo ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa shule ya upili ya Chavakali kaunti ya Vihiga alifariki kwenye ajali. Ajali hiyo ilitokea katika makutano ya Mamboleo kaunti ya  Kisumu mnamo Aprili 1, 2024.

Ibada ya mazishi ya Mwanafunzi wa Shule ya Upili ya Chavakali Joseph Mwadulo mnamo Ijumaa, Aprili 12, 2024. 

Waombolezaji walikutana katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Chuo Kikuu cha Kenyatta kabla ya kuelekea Embu kwa ibada ya kanisa na kisha kuelekea eneo la maziko.

Sherehe ya mazishi ilihudhuriwa na familia, marafiki, walimu, na wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Chavakali ambapo mtoto huyo wa miaka 17 alikuwa akisoma.

 Watu maarufu waliohudhuria ni pamoja na Jacque Nyaminde - Wilbroda Shirandula, Nyambura Wa Kabue, Shix Kapienga - Tasha, Wanjiku The Teacher, Njeri ithaga riene, Jose Gatutura, Terence Creative, Kamoko Wanjiru Waya Joyce na Wamamaa Wanja asali Mtoto wakiambulia. Mwadulo alipata ajali ya barabarani akitokea shuleni.