Nenda vizuri kaka!- Eric Omondi avunja kimya kufuatia kifo cha kakake mdogo

Eric alimuombea kaka yake apumzike kwa amani.

Muhtasari

•Huku akimuomboleza kaka yake, Eric alichapisha video ya wimbo wa kejeli ya kisiasa ambao walifanya pamoja wakati fulani nyuma.

•Eric na Fred walikuwa ndugu wa karibu sana na wote wawili walifanikiwasana katika tasnia ya burudani ya vichekesho.

katika picha ya maktaba
Fred Omondi na Eric Omondi katika picha ya maktaba
Image: HISANI

Mchekeshaji na mwanaharakati maarufu wa Kenya Eric Omondi yuko katika hali ya majonzi kufuatia kifo cha mdogo wake Fred Omondi.

Fred aliaga dunia siku ya Jumamosi asubuhi baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani katika Barabara ya Outering, jijini Nairobi.

Huku akimuomboleza kaka yake kwenye Instagram, Eric alichapisha video ya wimbo wa kejeli ya kisiasa ambao walifanya pamoja wakati fulani nyuma.

Kisha akamuombea kaka yake apumzike kwa amani.

“Nenda vizuri kaka @fredomondi_,” Eric aliandika chini ya video hiyo na kuiambatanisha na emoji ya moyo uliovunjika, kuashiria hisia zake kwa sasa.

Eric na Fred walikuwa ndugu wa karibu sana na wote wawili walifanikiwasana katika tasnia ya burudani ya vichekesho.

Polisi walisema ajali iliyomuua Fred ilitokea Jumamosi asubuhi baada ya bodaboda iliyokuwa imembeba kugongwa na basi lililokuwa likienda mwendo kasi na kumlazimisha mwendeshaji huyo na marehemu kutua kwenye lami.

Omondi alikimbizwa katika Hospitali ya Mama Lucy ambapo alitangazwa kuwa amefariki alipokuwa akihudumiwa, afisa wa polisi alisema.

Shahidi alisema alifariki papo hapo.

Marafiki na watu mashuhuri waliotumbuiza naye walikusanyika kwenye mitandao ya kijamii kuomboleza kifo chake.

Mchekeshaji Terrence Creative alipokuwa akimuomboleza alisema alipokea simu saa kumi na mbili asubuhi Jumamosi kumjulisha kifo chake.

"Fred namshukuru Mungu kwa muda aliotupa pamoja bro, umekuwa sehemu ya kazi yangu na ukuaji katika tasnia. Ulinichukulia kama kaka na kunikaribisha wakati sikuwa na mahali pa kwenda," Terrence alisema.

"Ulinipa jukwaa na kunilipa, na kwa pamoja tulianza maonyesho ya vichekesho vya klabu. Nitathamini kila wakati tuliposhiriki jukwaa."

Mwanasiasa Millicent Omanga, alitoa rambirambi zake kwa X, akisema:

"Tasnia ya ubunifu imepoteza thamani. Fred Omondi aliangaza vyumba vyetu vya kuishi na vichekesho vyake vya uraibu. Kwamba amepoteza maisha yake katika ajali ya barabarani inahuzunisha moyo. Ninawapa pole familia yake, marafiki, na mashabiki wake. Naomb nafsi yake ipate amani kamili."

Mwanamuziki Nameless naye alimlilia.

“Hii imezidi... maisha ni tete! Pumzika vizuri Fred! Habari za kusikitisha kama hizo! Pole za dhati kwa familia!!