Akothee aweka wazi wanaume ambao amewahi kutoka nao kimapenzi

Mwimbaji huyo ameweka wazi kuwa kamwe hajawahi kucheat katika mahusiano yake yote.

Muhtasari

•Akothee amesema amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume watano pekee ambao amewahi kuchumbiana nao.

•Aliwashutumu wanamtandao wengine Wakenya kwa kuwa na machungu na wivu juu ya maisha ya watu waliofanikiwa.

Akothee
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Akothee ni mwanamke mwenye ghadhabu kubwa baada ya kushutumiwa kwa kutokuwa na utulivu na kuwa na tabia ya kuruka kutoka mahusiano moja hadi mengine.

Katika machapisho yake ya hivi punde, mama huyo wa watoto watano amekuwa akiashiria hasira yake dhidi ya vyombo vya habari na wanamitandao ambao amewashutumu kwa kuchora picha mbaya kumhusu.

Mwimbaji  huyo mwenye umri wa miaka 42 amesema tofauti na wanawake wengine wengi, yeye amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume watano pekee ambao amewahi kuchumbiana nao.

"Nina miaka 40 na wanaume 5, hesabu jinsi nilivyo na nidhamu. Tena sicheat katika mahusiano yangu. Mimi huchumbiana na mwanaume mmoja mmoja, na mume wa mtu ni kidonge kichungu kwangu. Napenda mwanaume wangu tu," alisema kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Akothee alitoa ufafanuzi huo wakati alipokuwa akijibu tuhuma za kuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mzungu wa Afrika Kusini.

Alisema mwanamume huyo anayeonekana naye kwenye picha ambayo imekuwa ikivuma kwenye mitandao ya kijamii alikuwa ni vixen tu kwenye video yake ya muziki na hawakuwahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi.

"Yupo kwenye ndoa yenye furaha na ana watoto. Ni nini mbaya na nyinyi? Mnaweza kuwa na akili? Mheshimu familia za watu," alisema.

Aliwashutumu wanamtandao wengine Wakenya kwa kuwa na machungu na wivu juu ya maisha ya watu waliofanikiwa kama yeye.

Aidha, mjasiriamali huyo shupavu alisema kuwa yeye ni onyesho tu la kile kinachotokea katika jamii, tofauti ni kwamba watu wengine hawajaangaziwa sana kama yeye  kwa sababu wao sio watu mashuhuri.

"Mimi ni bora kuliko wanawake wanaocheat katika mahusiano sumu, sikubaliani na upuuzi. Sheria zangu ,kama sio za maana kwetu ,tunaacha.Sitakuwa na wanaume 6 maishani mwangu ili kutimiza sehemu zangu zingine nilizokosa.NAMPENDA MWANAUME MMOJA KWA WAKATI," alisema mwanamuziki huyo.

Kufikia sasa, Akothee amekuwa katika mahusiano matano yanayojulikana. Aliwahi kuwa kwenye ndoa na Bw Jared Okello ambaye ni baba wa binti zake watatu kabla ya kutalikiana na kuchumbiana na  wazungu wengine wawili ambao alizaa nao mtoto wa kiume kila mmoja.

Baadaye alijitosa kwenye mahusiano na aliyekuwa meneja wake, Nelly Oaks kabla ya kutengana katika hali tatanishi mapema mwaka huu. Kwa sasa anachumbiana na mzungu kutoka Uswizi ambaye amembatiza jina Bw Omondi.