Betty Kyallo atoa ujumbe maalum kwa dada yake mdogo akiadhimisha siku ya kuzaliwa

Betty alimhakikishia kwamba anajivunia maendeleo yake maishani.

Muhtasari

•Gloria alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 22 kwa njia maalum huku akiandamana na baadhi ya wanafamilia wake akiwemo Betty hadi kwenye jumba la burudani.

•Mtangazaji huyo pia alimhakikishia dadake kwamba yeye na binti yake Ivanna wanampenda sana.

Betty Kyallo na dada yake Gloria Kyallo
Image: INSTAGRAM// GLORIA KYALLO

Dada mdogo wa mjasiriamali Betty Kyallo, Betty Kyallo atoa ujumbe maalum kwa dada yake mdogo

Gloria ambaye ndiye mdogo kati ya dada watatu wa Kyallo alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 22 kwa njia maalum huku akiandamana na baadhi ya wanafamilia wake akiwemo Betty hadi kwenye jumba la burudani.

Huku akimsherehekea dadake kwenye Instagram, Betty alimhakikishia kwamba anajivunia maendeleo yake maishani.

"Ninajivunia mwanamke ambaye unamkuwa Bi. Usiruhusu ulimwengu uwahi kubadilisha hali yako ya upole, upendo wako kwa watu na mbwa waliokuzingira, tabia yako nzuri na shauku ya kujisukuma," aliandika.

Mtangazaji huyo pia alimhakikishia dadake kwamba yeye na binti yake Ivanna wanampenda sana.

"Kheri ya siku ya kuzaliwa mpendwa. Tusherehekee," alisema.

Betty aliambatanisha ujumbe wake na picha nzuri kadhaa za dada huyo wake mdogo. Kwenye Instastori zake, alionyesha baadhi ya matukio ya karamu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Bi Gloria.

Takriban miezi sita iliyopita, Gloria aliandaa sherehe za kukaribisha mtoto wa mbwa wake ambaye alikuwa mjamzito, kwa lugha ya kimombo ‘Puppyshower’, mfano wa ile ya binadamu ya ‘Babyshower’

Kyallo aliarusha tamasha la kifahari ambalo lilihudhuhiriwa na marafiki wake wa karibu kusherehekea ujauzito wa mbwa huyo wake aina ya Chiwawa.

Akitetea hatua yake, Gloria aliwajibu mashabiki wake waliokuwa wanamsimanga kwa kuandaa tafrija kwa ajili ya uzauzito wa mbwa kwa kuwaambia kwamba si vibaya kuwasherehekea Wanyama kwani huwa wanaonesha binadamu mapenzi ya dhati.

“Washerehekee Wanyama wenu kwa sababu wao ndio huwa na mapenzi ya kitiifu kikweli,” alisema.

“Msichana wa saa. Hongera kwa kusherehekea kila baraka. Ninampenda sana msichana huyu. Anastahili haya na mengineyo!! Hongera sana msichana wangu Lulu kwa kupata ujauzito wake za kwanza, Gloria Kyallo aliandika katika moja ya picha ya mbwa huyo aliyeuwa amemvalisha nguo kama mdoli vile.