Orodha ya wasanii ambao nyimbo zao zilitolewa kwenye Youtube kwa madai tofauti

Muhtasari
  • Orodha ya wasanii nyimbo zao zilitolewa kwenye Youtube kwa madai tofauti
Sailors-3-551x600
Sailors-3-551x600

Licha yao kutumia pesa nyingi kutoa kibao, wamekuwa upande mbaya  na mitandao ya kijamii ya youtube baada yao vibao vyao kuvuma sana kisha vinatolewa kwenye mitandao hiyo kwa madai tofauti.

Hivi juzi msanii Mejja aligadhabishwa na kitendo hicho baada ya kibao chake  cha 'Tabia za wakenya' kutolewa kwenye mitandao hiyo.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alisema kwamba hata kata tamaa na kwamba Mungu yuko.

Kaika makala haya nitakupa orodha ya wasanii ambao vibao vyao vilitolewa Youtube, huku nyingi zikiwa ni kwa madai ya hakimiliki.

1.Diamond Platnumz na Zuchu

Staa huyo alitoa kibao akimshirikisha msanii Zuchu, kibao cha 'jeje' kilitolewa kwenye youtube kwa maswala ya hakimiliki ya msanii Anthony Tony.

2.Mejja 

KIbao chake cha 'tabia za wakenya' kilitolewa youtube wiki jana kwa swala tu la hakimiliki.

3.Harmonize

KIbao cha msanii huyo cha 'uno' kilitolewa kwenye youtube siku chache baada ya kuwekwa mitandaoni.

Hii ni baada ya producer kutoka Kenya Magix Enga kudai baadhi ya midundo imetolewa kwa kibao chake.

4.Sailors

Miongoni mwa vibao vya bendi hiyo ya gengetone ambavyo vilitolewa youtube ni Chebukati miongo mwa vingine.