Aibu!Diamond Platnumz awashambulia wanaoeneza chuki kati yake na msanii Alikiba

Muhtasari
  • Kupitia kwenye mitandaoya kijamii ya Instagram Diamond amewakashifu mashabiki ambao wanawalinganisha wasanii
  • Diamond Platnumz awashambulia wanaoeneza chuki kati yake na msanii Alikiba
Mwanamziki Diamond Platnumz
Mwanamziki Diamond Platnumz
Image: HISANI

Chuki,ugomvi n a vita za maneno zimekuwa zikishuhudiwa kwenye tasnia ya burudani kila kuchao kati ya wasanii.

Staa wa bongo Diamond na msanii wa bongo Diamond Platnumz na  Alikiba wamekuwa kama hawasikizani kwa muda sasa.

Kupitia kwenye mitandaoya kijamii ya Instagram Diamond amewakashifu mashabiki ambao wanawalinganisha wasanii badala ya kuwaunga mkono.

Kwenye ujumbe wake aliwaambia mashabiki kwamba wanaharibu wakati wao mwingi kwa kuunda chuki badala ya kusaidia nyiimbo zao ili washindane na wasanii kutoka nchi za nje na kulete heshima katika nchi yao.

KUlingana na baadhi ya mashabiki na wanamitandao ujumbe huo ulikuwa unaendea mashabiki wa Tanzania ambao wamekuwa wakieneza chuki kati yake na Alikiba.

Mapema wiki hii wasanii hao wametoa kibao kila mmoja na mashabiki wao wamo mbioni kuangalia ni kipi kitakuwa na watazamaji wengi kwenye youtube.

"Mnapoteza muda wenyu mwingi katika kuchonganisha wasanii,wenu watanzania ili wagombane badala ya kutumia muda huo kuwapromote

Ili tukashundane na wenzetu wa maitafa wenginena kuleta heshima katika taifa letu...Aibu." liandika