Ringtone pole sana sina mimba yako,'Kipusa aliyedai kuwa na ujauzito wa Ringtone aomba msamaha

Muhtasari
  • Kipusa aliyedai kuwa na ujauzito wa Ringtone aomba msamaha
Ringtone Apoko
Ringtone Apoko
Image: Hisani

Kipusa anayefahamika kwenye mitandao ya kijamii kama Akuju Mbosso ametafuta umaarufu kwa njia zozote, ata kwa kutafuta kiki na kumwekelea msanii Ringtone alimpa ujauzito.

Wiki chache zilizopita alidai kwamba ana ujauzito wa msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko.

Ni jambo ambalo msanii huyo hakulizungumzia wala kusema kuhusu madai hayo.

Kupitia kwenye ukurasa wa Akuju wa instagram aliomba msamaha na kudai kwamba aliambiwa aseme hayo na 'producer' mmoja ambaye alitaka kumharibia msanii huyo jina.

Kipusa huyo alidai kwamba hana mimba ya msanii huyo na akamuomba msamaha.

Ujumbe;

"Nimelazimika kuomba msamaha hadharani kwa maana nilimwaribia ringtone jina hadharani kwa kusema kwamba alnipa ujauzito,nilishawishiwa na mzalishaji aliyeniahidi nita rekodi kibao moja bila malipo baada ya kuchomea uyo jamaa.najua haujaelewa kizungu,RINGTONE APOKO pole sana sina mimba yako ni kiherehere tu,am sorry," Aliandika Akuju.