Nimekusamehe!Ringtone amsamehe kipusa aliyedai ana ujauzito wake

Muhtasari
  • Ringtone amsamehe kipusa aliyedai ana ujauzito wake
  • Wiki chache zilizopita alidai kwamba ana ujauzito wa msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko
Ringtone Apoko
Ringtone Apoko
Image: Instagram

Kipusa anayefahamika kwenye mitandao ya kijamii kama Akuju Mbosso ametafuta umaarufu kwa njia zozote, ata kwa kutafuta kiki na kumwekelea msanii Ringtone alimpa ujauzito.

Wiki chache zilizopita alidai kwamba ana ujauzito wa msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko.

Siku ya JUmamosi kipusa huyo aliomba msamaha hadharani na kudai kwamba haikuwa kupenda kwake kusema hayo na kumwaribia msaniin wanyimbo za injili Ringtone Apoko jina.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Akuju alimuomba msanii huyo msamaha, ambapo Ringtone alisema kwamba amemsamehe.

"Mungu huw anasamehe dhambi zote,na mimi kama mwana wake nitamsamehe mwana daa huyu machozi yangu Yesu atayaoangusa,"Ringtone Aliandika.

Kipusa huyo alidai kwamba hana mimba ya msanii huyo na akamuomba msamaha.

"Nimelazimika kuomba msamaha hadharani kwa maana nilimwaribia ringtone jina hadharani kwa kusema kwamba alnipa ujauzito,nilishawishiwa na mzalishaji aliyeniahidi nita rekodi kibao moja bila malipo baada ya kuchomea uyo jamaa.najua haujaelewa kizungu,RINGTONE APOKO pole sana sina mimba yako ni kiherehere tu,am sorry," Aliandika Akuju.