'Hatutaachana,'Weezdom asema baada ya kurudiana na mpenzi wake

Muhtasari
  • Mahabiki wazua mdahalo mitandaoni baada ya Weezdom kurudiana na mpenziwe
Image: Maktaba

Jumatatu, Weezdom  kwenye mitandao ya kijamii alitangazia ulimwengu na mashabiki  kwamba alikuwa amerudiana na mpenzi wake wa zamani Mylee Staicey.

Wawili hao walitengana mnamo Januari mwaka huu, lakini wamerudi pamoja.

"Morning Guyysss Ambieni Kamati ya Roho Chafu, Weez & @mylee_staicey wamerudi😊#HatutaachanaTuu," Aliandika Weezdom.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mylee Staicey ambaye pia alishiriki picha ya kutuliza na staa huyo wa zamani wa Injili, akisema kuwa Upendo wa Kweli haufi kamwe.

"True love never dies @weezdom254 ❤️Changu ni changu,wana pambana sanaaaa😂😂😂," Aliandika Stacy.

Ni hatua ambayo wengi wa wanamitandao waliipongeza na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

yycomedian: Sisi kama kamati ya roho chafu we deny the allegations...we didn't participate in the separation...It was a collateral damage matter 😂

janetotienoke: Watoto Wangu mmechagua fungu jema. Lunch is almost ready ❤️💖

nanaowiti: Alaaaaa!! Aki mtanionyesha mambo 😮

chriskirwa: Nyinyi ndio muliachana Sisi tunajua you are item for alwaysJipangeni 😀😀

sindamatiko: Hamjiskii kufungua YouTube Channel

africanbeamer: walai umetucheza miezi mob😂😂😂

maureen.muthoni.900: Awww❤️ Mylee am so happy for you now fight for your love ❤