Nilianza kazi ya ukahaba baada ya kudhulumiwa kingono na mjomba wangu-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Kuna baadhi ya mambo ambayo wengi walitendewa utotoni mwao  na kuanza kazi ambayo haistahili
kahaba 1
kahaba 1

Kuna baadhi ya mambo ambayo wengi walitendewa utotoni mwao  na kuanza kazi ambayo haistahili.

Sio wote ambao wamebahatika kulelewa na wazazi wao kuna wale wamepitia mikononi mwa mama au baba wa kambo,shangazi au wajomba wao.

Baadhi yao walichukua faida hiyo na kuwadhulumu kimaisha, huku wengi wakikata tamaa ya kuishi.

Kazi ya ukahaba ni moja wapo ya kazi ambazo huonekana hazistahili na kazi za kinyume cha sheria nchini.

NIkiwa katika ziara yangu, nilipatana na mwanamke mmoja ambeye alinisimulia sababu yake ya kuanza kazi ya ukahaba.

Je sababu ni ipi?

"Mimi si kubahatika kulelewa na wazazi wangu, na mama yangu alinizaa kama hajaolewa baada ya miaka 7 aliaga dunia

Aliniacha kwa mjomba wangu, yaani ndugu yake ili aweze kunisaidia, sikufahamu kumbe mjomba wangu alikuwa amepata nafasi ya kunidhulumu

Alianza kunidhulumu nikiwa na miaka 11, kumwambia shangazi yangu aliniambia kwamba ni mimi mwenye makosa ilhali sikuelewa makosa yangu

Nilitoroka nyumbani na kuenda mjini, sikuwa na jambo lolote la kufanya,nilikuwa chokora kwa muda baada ya kuhitimu miaka 19 nilijiunga na kazi ya ukahaba

Wasichana wengi wanafanya kazi hiyo, walikosa namna ya maisha, na wengine wanahepa nyumbani kwa ajili ya mateso ambayo wanapokea," Alisimulia mwanamke huyo.

Mwanamke huyo alifichua kwamba amekuwa akifanya kazi hiyo sasa kwa zaidi ya miaka 20.

"NI jambo ambalo sitawahi msamehe mjomba wangu, kwa maana hajawahi nitafuta baada ya kutoroka ni kama nilikuwa takataka kwake

Kwa sasa nimeacha kazi hiyo, nafanya biashara yangu, na sidhani kwamba nitawahi fanya kazi hiyo tena, kwa maana changamoto ni nyingi sana

Sijuti kufanya kazi hii kwani ndio imefanya niweke biashara ambayoo inaniletea mkate wa kila siku."