Nilitoroka nyumbani baada ya wazazi wangu kutaka kunioza kwa baba mzee-Kipusa asimulia

Muhtasari
  • Kipusa atoa sababu ya utoroka nyumbani kwa zaidi ya miaka 15
Side view of young woman with eyes closed
Side view of young woman with eyes closed

Utamaduni uifuatwa sana wakati wa akina babu zetu, huku karne ya sasa ikitawala utamaduni, kama bile kuozwa mapema na wazazi wako.

Baadhi ya akina mama zetu waliozwa wakiwa na umri wa chini na wazazi wao kwani walikuwa na sababu tofauti.

Kuna wale ambao walieweza kuozwa kutokana na umaskini ili familia itajirike na wale waliozwa ili wasilete aibu katika familia.

Nikiwa katika ziara zangu nilipatana na mwanamke mmoja aliyefahamika kama Chumo ambaye alisimulia hadithi yake kwa nini alitoroka nyumbani kwao.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nilipohitimu miaka 14, baba yangu alikuwa mpenda utamaduni na mila sana, alisema kwamba siwezi endelea na masomo kwani nilikuwa nimefikisha umri wa kuolewa kulingana naye

Cha kushangaza ni kuwa hakuwa anataka kunioza kwa mwanamume mwenye umri wa kati, bali alikuwa anataka kunioza kwa baba mzee ili apate pesa

Si kusubiri hayo yatendeke, nilitoroka nyumbani kwa maana sikuwa nataka kuozwa nilikuwa nataka kuendelea na masomo, sasa ni zaidi ya miaka 15 sijawahi rudi nyumbani kwa sababu si kutaka kuwaona wazazi wangu

Baada ya kutoroka nilianza kufanya kazi kama kijakazi, mpaka mahli nilipo sasa nimeanzisha biashara yangu

Nilikuwa nataka ushauri je nirudi nyumbani nikawaone wazazi wangu na tuombane msamaha, kwa sababu huwa nazungumza na ndugu zangu, licha ya kuenda kinyume na matarajio ya baba yangu

Na jambo lingine nimepeza wazazi wangu licha ya yale walinifanyia, mzazi ni mzazi," Alisimulia Chumo.

Je ushauri wako kwa mwanadada huyu ni upi?