Ambieni serikali iwape kazi,'Akothee kwa wanaosubiri aachane na mpenzi wake

Muhtasari
  • Haya basi madam Boss amezungumza na kukomesha wanaosema na kudai kwamba uhusiano wake na mpenzi wake hautadumu
Nelly Oaks na Akothee
Nelly Oaks na Akothee
Image: INSTAGRAM//NELLY OAKS

Haya basi madam Boss amezungumza na kukomesha wanaosema na kudai kwamba uhusiano wake na mpenzi wake hautadumu.

Kulingana na Akothee wanaotarajia waachane basi waambie serikali iwape kazi, na kama wamesimama wanapaswa kuketi.

Uhusiano wake Akothee na Nelly ulikejeliwa na baadhi wa wanamitandao baada ya kutangaza kwamba wawili hao ni wapenzi.

Pia aliwaambia wanaokejeli uhusiano wake kwamba wanapaswa kushughulikia maisha ya kwao na wala sio ya kwake.

"Kwa wale wanangoja machozi,nawashauri mnapaswa kuambia serikali iwape kazi,hii linawea kuchukua muda

Na kama umesimama tafdhali chukua kiti na uketi, sitaki misuli yao ichoke, kondeshwa na ya kwako

Kuwa single mther haimaanishi kwamba utaacha kujipenda,chumbia mtu yeyote ambaye unataka kuchumbia, lakini hakikisha familia yako iko sawa

Acha kunifuata kwa upofu, shirikisha akili zingine," Aliandika Akothee.

Haya basi kwa wale walikuwa wanasubiria Akothee aachane na mpenzi wake amewataarifu kwamba yatachukua muda.