Singekuwa na mtu ambaye ni mbaya kwangu,nilionywa dhidi ya kumchumbia Vera-Jimmy Chansa

Muhtasari
  • Hata hivyo amesema kwamba aliamua kufuata moyo wake na  kufanya maamuzi kama mtu mzima
Vera Sidika na Jimmy Chansa
Vera Sidika na Jimmy Chansa
Image: Hisani

Aliyeuwa mpenzi wa zamani wa mwanasoshalaiti Vera Sidika, Jimmy Chansa, akiwa kwenye mahijiano amesema kwamba alikuwa ameonywa dhidi ya kumchumbia Vera.

Hata hivyo amesema kwamba aliamua kufuata moyo wake na  kufanya maamuzi kama mtu mzima.

Awali akiwa kwenye majoniano Chansa alifichua sababu kuu ya kutompa Vera Ujauzito akisema kwamba ni jambo ambalo halikuwa kipaumbele katika uhusiano wao.

"Ni kawaida, na mimi ni mtu mzima siwezi kuwa na mtu ambaye ni mbaya kwangu, Mimi sifuati sana comments za social media, lakini kama mwanadamu kuna watu walikuwa wanasema coz wanamjua kupitia mitandao ya kijamii. watu walimuona kama mtu ambaye alikuwa wa bei ghali, lakini mimi nilimuona kama mpenzi wangu,hisia ni tofauti," Alisema Chansa.

Aliendelea kusema kuwa anaweza kupata mtoto na mwanamke ikiwa anataka.

"Ikiwa ninataka mtoto, nitampata."

"Kuna watu bilioni nane ulimwenguni na sio wakati wangu wa kupata mtoto. Mungu ndiye anayewapa watoto.

Kwangu kupata mtoto sio kipaumbele kwa sasa. Ikiwa wakati utafika, kuna takriban wanawake bilioni nne katika dunia." Alisema awali alipokuwa kwenye mahojiano.

Ni Mtanzania Jimmy Chansa ambae time hii amefanya mahojiano na Ayo TV kueleza yale tusiyoyajua kuanzia kuvunjika kwa penzi lake na mrembo Vera Sidika pamoja na mengineyo tusiyoyafahamu.

Pia amesema kwamba kuachana Afrika inachukuliwa kama jambo, mabaya ilhali  ni jambo la kawaida.