Chimano wa Sauti Sol akiri 'kupenda wanaume'

Muhtasari

• Chimano alikuwa hajawahi kujitokeza hadharani kama mpenzi wa jinsia moja ingawa hapo awali aliwahi kuonekana na wapenzi wa kiume.

chimano
chimano

Star wa Afro-Pop nchini Kenya na ambaye anaimba na bendi ya Sauti Sol Chimano amekiri kwamba yeye anapenda wanaume wenzake.

Tamko la hadharani la Chimano lilikuja alipokuwa akielezea wazo la wimbo wake mpya, Friday Feeling, ambapo aliwashirikisha wanajamii wa LGBT.

"Hakuna kujificha tena," aliambia vyombo vya habari nchini Kenya.

Alisema kwa sasa anaishi maisha yake atakavyo na kwamba atatumia muziki wake kupinga unyanyapaa dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, chuki na unafiki.

Chimano alikuwa hajawahi kujitokeza hadharani kama mpenzi wa jinsia moja ingawa hapo awali aliwahi kuonekana na wapenzi wa kiume.

Tamko hilo la hadharani linaweza kuwa kupiga jeki juhudi za kupigania haki za watu wa jamii ya LGBT nchini Kenya, ambapo mapenzi ya jinsia moja yameharamishwa na yanaweza kuadhibiwa kwa hadi miaka 14 jela.

Kulingana na watafiti jamii ya wapenzi wa jinsia moja inazidi kuongezeka nchini Kenya huku baadhi ya mashirika ya kimataifa yakishinikiza kuhalalishwa kwa mahusiano ya jinsia moja nchini Kenya.