Willy Paul atangaza azma yake ya kuwania kiti cha ubunge mwaka ujao

Muhtasari

•Paul ambaye hivi karibuni amekuwa akivuma kwenye mitandao yote ya kijamii kufuatia drama mbalimbali zilizomkabili alitangaza azma yake ya kuwania kiti cha ubunge cha Mathare kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Mwanamuziki mashuhuri Wilson Abubakar Radido almaarufu kama Willy Paul ndiye msanii wa hivi punde kuonyesha nia yake ya kujitosa kwenye siasa.

Paul ambaye hivi karibuni amekuwa akivuma kwenye mitandao yote ya kijamii kufuatia drama mbalimbali zilizomkabili alitangaza azma yake ya kuwania kiti cha ubunge cha Mathare kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

"Je, mko tayari Mathare? Tulete mabadiliko hayo," Willy Paul aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha ya bango lenye sura yake na maandishi "Willy Paul, Mathare MP 2022."

Willy Paul hata hivyo hakutangaza chama ambacho anatazamia kutumia kuwania kiti hicho ambacho kwa sasa kimekaliwa na anthony Tom Oluoch

Wanamitandao walipokea hatua ya msanii huyo asiyepungukiwa na sarakasi katika taaluma ya muziki kwa hisia mbalimbali.

@colloh_001 wewe tuimbie tu wachana na Siasa

@martinkihia Umekosea.. Mathare hospital

@duke_kibiwotrodgers Haiyaa, MP  inataka Degree, lakini mbinguni hakuna Degree.

@cool_kid dennoh Am voting for you

@iamcalvin01 Si wewe ndio ulisema mwanamuziki akianza siasa huwa ameishiwa na content.. tunaweza kudhubitisha