Mkewe Samidoh ajibu madai ya Karen Nyamu alimsaidia kupata zabuni ya milioni 9

Muhtasari
  • Mkewe Samidoh ajibu madai ya Karen Nyamu alimsaidia kupata zabuni ya milioni 9

Mkewe Samidoh amejibu madai ya Karen Nyamu kwamba alimsaidia kupata zabuni ya Ksh 9 Milioni

Ugomvi kati ya Karen Nyamu na mke wa Samidoh Edday ulichukua mkondo mpya wiki jana baada ya Edday kufichua Seneta anayempendelea zaidi wa Nairobi.

Katika mitandao yake ya kijamii, mama huyo wa watoto wawili alisema anamuunga mkono Julie Kabogo anayewania chini ya Chama Cha Kazi Party.

Chapisho lake lilikuwa na maoni tofauti kutoka kwa mashabiki.

Shabiki aliyejulikana kama Muthoni Wakahiu Maina alimweleza kwamba anapaswa kuona haya kwa kutomuunga mkono Karen lakini alimsaidia kupata zabuni ya Ksh 9 milioni.

Edday alimjibu kwa kumwambia shabiki huyo kwamba afanye utafiti ili kujua ukweli na mara atakapopata ukweli afunge mdomo wake.

Muthoni Wakahiu Maina: Huna shukrani!) Baada ya kupewa zabuni ya milioni 9, Bado umemruka? Anyway... am team mbuzi mke! Julie njia yote!

Edday alimjibu kuwa:

Muthoni Wakahiu Maina wewe ni tender unapenda,uliona nikipewa,chunguza ukijua ukweli uache mdomo.

Nyamu, katika mahojiano na Jalang’o TV ambayo  yalifanyika mwaka jana alisema alimsaidia mke wa Samidoh kusajili kampuni iliyopata zabuni ya sh Milioni 9 akitupilia mbali madai kuwa yeye ni mhalifu.

“Tofauti na watu wanavyofikiri kuwa nataka kumtoa nje, mimi nimekuwa nikishiriki kusaidia familia, mwaka jana nilimpa wazo Samidoh kwamba yeye (mke wa Samidoh) asajili kampuni kwa sababu tulikuwa tunapata zabuni, sasa hivi yuko akihudumia zabuni ya vifaa vya kuandikia yenye thamani ya Sh9 milioni ambayo mimi na kaka yake Samidah Kariz Magic tuliketi na kufanya nyaraka hizo,” alidai Nyamu.

Je ugomvi kati ya wawili hao utakwisha, licha ya watoto wao kuwa na baba mmoja, na ni nani anasema ukweli?