Sikutoa mtu kafara,'Magix Enga afichua jinsi alivyojiunga na Illuminati

Muhtasari
  • 'Magix Enga afichua jinsi alivyojiunga na Illuminati
Magix Enga
Magix Enga

Idadi kubwa ya wasikilizaji wa Gengetone wanafahamu Magix Enga ni nani na kimsingi yeye ni mmoja wa watayarishaji maarufu mjini na pia msanii bora wa Kenya.

Tangu Gengetone kupoteza idadi ya wafuasi, wasanii wengi walipoteza umaarufu lakini inaonekana watu kama Magix Enga walibaki wamesimama.

Saa kadhaa zilizopita, mtangazaji Ali alikutana na Magix Enga katika tukio na akaamua kuwa na kipindi kimoja cha mazungumzo naye.

Alifichua kuwa katika tasnia ya burudani, kamwe si rahisi hivyo na lazima upate matatizo mengi unaposhindana na wapinzani ili kuwa bora.

Kuhusu umaarufu wake, Magix Enga alifichua kuwa nusura aingie mtegoni baada ya kudanganywa na rafiki yake kujiunga na illuminati.

Alisema kuwa rafiki huyo alimwambia kwamba atakusanya mali ndani ya muda mfupi lakini hakuwahi kumwambia kama kulikuwa na matokeo yoyote katika safari.

"Nilipatana na mwanamke ambaye alinihusisha na Illumnati, watu hawapaswi kutania Illuminati, lakini nikisema au kufanya kitu watu wanasema kwamba natafuta kiki, aliniambia kwamba nitakuwa tajiri kwa muda wa miezi miwili

Nilinunua gari ya kwanza, mambo yalikuwa yanaenda vyema, wakati nilipofanya ajali nikaomba mambo yalibadilika na kila kitu kikaisha."

Aliendelea;

"Yaani unapozidi kuomba ndio vitu ambavyo nilipokea vinaisha, wasanii wengi wa kenya wako huko,lakini nimeokoka

Sikuwahi toa mtu kafara nilijitoa mimi mwenyewe."

Aliwashauri vijana waepuke kutafuta fedha za kirahisi na wafanye kazi kwa bidii ili wapate mafanikio hata kama yatakuwa kidogo.

Enga alidai kwamba ameokoka na kwamba amemrudia Yesu, licha ya hayo yote.