"Baby wangu asante" Zuchu amsifia mpenzi wake

Zuchu
Zuchu

Mwanamuziki kutoka nchi ya Tanzania Zuchu amemsifia mpenzi wake baada  ya kumnunulia zawadi ambayo alikuwa anatamana sana.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram alichapisha video iliyoambatana na sauti yake, akieleza furaha yake baada ya kupokea zawadi ya mdoli aliyokuwa a al ameagiza kutoka kwa mpenzi wake.

Kwenye video hiyo,  ilikuwa inaonyesha mdoli aliyeletewa na mpenzi wake huku akionekana  mwenye bashasha isiyokuwa na kifani .

Zuchu alimshukuru mpenzi wake ambaye muda wote Zuchu amekuwa  akificha jina lake  kwa zawadi aliyompea.

Kulingana naye alitaka mpenzi wake amnunulie mdoli mkubwa, lakini alichokuwa hana uhakika nacho ni  kuwa hakutarajia kununuliwa mdoli mkubwa kiasi hicho.

Wafuasi wake walichangamkia video hio huku wakimtaka aseme ni mpenzi yupi alimletea zawadi hio. 

Ikumbukwe ni hivi majuzi Zuchu alitangaza kuwa yuko singo na hana haraka kujihusha na mahusiano. Hii ni baada ya kuibuka uvumi kwamba alikuwa na mahusiano na  bosi wake Diamond Platnumz.

Zifuatazo ni baadhi za maoni ya wafuasi wa mwanamuziki huyo;

@Romyjons- BABY GANI MWAYA MDOGO ANGU ZUU

@nomakatembo-Baby wako ni Nani anakuwa na utoto ...Kama diamond

@bienfaitcasinga- Hiyo kitu niliona kwenye Gari ya Daimond juzi kumbe ndo amekuzawadiya