'Hongera' Nicki Minaj ampongeza Rihanna kwa ujauzito

Muhtasari

•Mitandao yote ya kijamii ilisheheni habari moja tu, nayo ilikuwa ni Rihanna kuwa na Ujauzito, hadi wakati huu nilipokuwa ni andika habari hizi, msanii huyo alikuwa anatrendi nambari moja  kwenye mtandao wa twitter

•Nicki alitumia ukurasa wake wa instagram, kuchapisha picha iliyokuwa ikionyesha ujauzito wa Rihanna iliyoambatana na maneno ya kumpongeza na kumkaribisha kwa hatua nyingine ya maisha.

 

A$ap Rocky, Rihanna na Nicki Minaj
A$ap Rocky, Rihanna na Nicki Minaj

Jana habari za Rihanna kuonyesha ujauzito wake kwenye mtandao, Habari zilisambaa dunia nzima; si bara Afrika, si Marekani bali pia bara la Uropa.

Mitandao yote ya kijamii ilisheheni habari moja tu, nayo ilikuwa ni Rihanna kuwa mjamzito, hadi wakati huu nilipokuwa naandika habari hizi, msanii huyo alikuwa anatrendi nambari moja  kwenye mtandao wa twitter.

Rihanna  ni msanii wa kike ambaye anafuatiliwa sana na kizazi kipya na miongoni mwa wasanii wengi ambao wanawafuasi wengi duniani huku wengi wakisema sauti yake nyororo inaweza kumtoa nyoka pangoni.

Waliokuwa marafiki wake wa karibu, moja wao ni Nicki minaji hawajasazwa   na habari hizi huku wakijitokeza na kumpongeza  Rihanna kwa mimba yake.

Nicki alitumia ukurasa wake wa instagram, kuchapisha picha iliyokuwa ikionyesha mimba ya Rihanna iliyoambatana na maneno ya kumpongeza na kumkaribisha kwa hatua nyingine ya maisha.

Rihanna ambaye ana umri wa miaka 33 alipakua picha  ya ujauzito wake wakiwa na mpenzi wake,A$AP Rocky  ambaye alitajwa kuwa na furaha kubwa anapotarajia kifungua mimba.

Wengi wa mashabiki wa wapenzi hao walistaajabu  ya Musa kwani hawakuwa wametarajia habari kama hizo kwani hakuna tetesi zilizokuwepo za rihanna kuwa na mjamzito.