Mwanamuziki Profesa Jay alazwa hospitalini, mwandani wake azungumzia afya yake

Muhtasari

•Mwandani mmoja wa mwanamuziki huyo amethibitisha habari hizo kupitia kituo kimoja cha radio nchini humo

•Wasanii mbalimbali wametuma sala za kumtakia afueni Profesa Jay ambaye alikuwa mheshimiwa wa Mikumi.

PROFESA Jay
PROFESA Jay
Image: twitter/hisani

Msanii nguli wa Hip Pop Bongo, Joseph Haule almaarufu Profesa Jay  imeripotiwa kulazwa katika hospitali moja nchini humo.

Mwandani mmoja wa mwanamuziki huyo amethibitisha habari hizo kupitia kituo kimoja cha radio nchini humo.

Kulingana naye, afya ya Jay ilianza kudhoofika wiki jana ambapo walimpeleka hospitalini  na kushauriwa na madaktari wampeleke katika hospitali kubwa zaidi ambako alilazwa kwenye chumba cha ICU  kwa siku mbili.

"Tangu Jumatatu alikuwa hayuko freshi,alienda kuangalia pale hospitali ila akambia hali yake sio nzuri, ikabidi wamulanze ili wa mwangalie hali yake zaidi na wamfanyie utafiti zaidi, kutoka pale walilituma hospitali nyingine ambao aliwekwa kwa ICU  kwa siku mbili" alisema mwandani wa Profesa Jay.

Kupitia mtandao wa Global Publisher, wasanii mbalimbali wametuma sala za kumtakia afueni Profesa Jay ambaye alikuwa mheshimiwa wa Mikumi.

Miongoni mwa wasanii waliomtumia Jay jumbe za afueni ni Diamond Platnumz  akisema anamtakia afueni ya haraka.

Pia sisi tunaongana na wote waliomuombea profesa apone arudi kwenye tasnia ya muziki ambayo kila wakti uienzi na kusifia.